Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Nikiona ukurasa wako wewe unapenda sayansi. Karibu kuchangia hapa - kwa Kiswahili na kwa maneno yako (maana hatukubali kopi-paste, angalia mwongozo) Kipala (majadiliano) 10:51, 19 Machi 2017 (UTC)Reply

WILAYA YA KYELA MKOANI MBEYA

hariri
     IFAHAMU WIRAYA YA KYELA MKOANI MBEYA

Kyela ni moja ya wiraya zilizopo mkoa wa mbeya,Wiraya ya kyela ilianza kutambulika toka mwaka 1984 baada ya mfululizo wa matukio yaliyopelekea kuanzishwa chini ya kifungu cha sheria namba 7 (Act No. 7) (mamlaka ya wiraya) ya mwaka 1982. Wiraya ya kyela ipo kusini mwa mkoa wa mbeya pamoja na huo mkoa kuwa upande wa kusini kiujumla. Wiraya ya kyela inapakana na Wiraya ya Makete iliyopo mkoani Iringa, Wiraya ya Ludewa upande wa mashariki iliyopo Iringa, Upande wa magharibi inapakana na wiraya ya Ileje,na upande wa kaskazini inapakana na wiraya ya Rungwe, Lakini upande wa kusini mwa wiraya ya kyela inapakana na ziwa nyasa ambalo linaingia mpaka nchini Malawi.

KATA ZA WIRAYA YA KYELA • Bujonde • Busale • Ikama • Ikolo • Ipande • Ipinda • Kajunjumele • Katumba Songwe • Kyela Mjini • Lusungo • Makwale • Matema • Mwaya • Ngana • Ngonga • ikimba

TABIA YA NCHI

Wiraya ya kyela ipo bondeni na ufukweni mwa ziwa nyasa na inapata mvua za wastani wa 2000 – 3000mm kwa mwaka na msimu wa mvua ni kati ya mwezi novemba mpaka juni,lakini Mwezi wa nne na wa tano kunakuwa na mvua nyingi zaidi.

Wiraya ya kyela ina hali ya joto wastani wa 23°C na uoto wa asili ni wa savanna misitu na nyasi na maji mengi majaruba pamoja na mabwawa,lkn pia kuna uwepo wa mito.

Ziwa nyasa ni moja ya ziwa kubwa lipatikanalo wirayani hapo ambalo linaunganisha nchi kama MALAWI,TANZANIA,MSUMBIJI, Wiraya ya kyela pia inapitiwa na mito mikubwa minne ambayo ni SONGWE, MBAKA, LUFILYO na KIWIRA na mito midogo kama mkalizi, kampala, mgaya, chiji, kandete,masukila, njisi,na kubanga. Vyanzo vingine vya maji wirayani hapo ni pamoja na ziwa Kingili, na chemichemi za maji moto kilambo.

Misitu inachukua takribani hekta 29,433 wirayani hapo na maneo ambayo yapo katika hifadhi ya serikali ni kama Busale, Ikomelo, Kabulo, Kasumulu, Safu za milima livingstone, Lugela, Nakaba, Kigalimu, Masoko na Masukulu.

KILIMO

Wiraya ya kyela ndo wiraya pekee inayozalisha mpunga au mchele pekee maarufu hapa nchini, mchele wa kyela unapatikana karibia kila soko lililopo hapa nchini, pia kuna wanafanya biashara wanatumia jina la mchele wa kyela kama matangazo wa biashara zao za mchele hata kama mchele wanaouza sio wa kyela, na hii ni kutokana na ubora wa mchele huo.

Na zao lingine linalopatikana wiraya ya kyela ni KAKAO. kakao ni zao kubwa la biashara wirayani kyela. Na wirayani kyela yanapatikana pia matunda kama maembe, machungwa,ndizi,nanasi,maparachichi, nazi.

Wirayani kyela hamna kiwanda kikubwa zaidi ya viwanda vidogovidogo pamoja na uhitaji mkubwa wa viwanda kutokana na mazao yanayozalishwa wirayani hapo.

UTALII

Uwepo wa ziwa nyasa wirayani hapo kumesababisha kuwepo kwa fukwe nyingi kama MATEMA, KAFYOFOYO, KAJUNJUMELE, NGONGA, BUJONDE na MWAYA. Na hizo ni fukwe nzuri zaidi afrika mashariki.


Pia kuna vijiji kama IKOMBE, LYULILO ambavyo ni maarufu kwa utengenezaji wa vyungu bora ambavyo vinasambazwa Tanzania nzima kwa ajili ya kupikia.

UTAMADUNI

Kabila kubwa lipatikanalo wirayani kyela ni wanyakyusa ambapo imeonekana wanawake ndio wanaoonekana kufanya kazi ya kutunza familia kuliko wanaume.

Pamoja na kuwa wanawake wana mchango mkubwa katika familia zilizo nyingi lakina mwanaume ndio mtoaji wa maamuzi zaidi katika familia. --DONALD MAHAMBA (majadiliano) 08:04, 26 Machi 2017 (UTC)Maandishi ya italikiMaandishi ya italiki'Reply