Karibu Wikipedia ya Kiswahili! --Chamdarae 00:03, 16 Desemba 2005 (UTC)Reply

Asante kwa ajili ya makala kuhusu Tanga! Lakini siamini ya kwamba asili ya jina "Tanga" ni lugha ya Kiajemi. Habari hii imepatikana wapi? --Kipala 18:19, 25 Desemba 2005 (UTC)Reply

Asante kwa jibu. Labda tuhame kwenye ukurasa ya majidiliano ya Tanga - ni afadhali kupeana jibu --Kipala 18:32, 25 Desemba 2005 (UTC)Reply


Salamu! Nisipokosa umeniuliza swali lifuatalo (lakini umesahau kuweka sahihi yako > ni kitufe cha pili hapo juu kuanzia kulia, ukifungua "hariri" - --172.178.129.173 21:58, 7 Januari 2006 (UTC)Reply

Habari ya mwaka mpya!
Samahani ninaomba tusaidiane kuupata ukweli, kitabu cha The story of East Africa and it's stamps kilichoandikwa na James A. Makay Kimeandikwa; Uganda ina maili za mraba 93,980 na katika Jarida la National Geographic la November 1971 limeandikwa; Uganda ina maili za mraba 91,134. Ahsante,

--Joel Niganile 09:06, 11 Januari 2006 (UTC)Joel NiganileReply

Mwaka mpya salama. Sasa wanipa ugumu ukianza mambo ya maili; mimi ni mtu wa mita. Nimeangalia kamuzi elezo zangu mbili zilizoko kwa CD:
Encycl. Britt. inasema : 93,072 square miles (241,038 square km), na MS Encarta inasema: 241 038 km².
Kwa sababu zinalingana zote mbili, ningeenda na hiyo lakini kwa kutaja km². --Kipala 19:24, 7 Januari 2006 (UTC)Reply


Joel hujambo! Nimefurahi kukuona tena! Ombi tu: kwanza endelea, halafu jaribu kukumbuka kazi ya viungo!!! Bila hii kazi itakuwa bure kwa sababu hakuna mtu atakayeona makala yako. --Kipala 19:32, 10 Julai 2007 (UTC)Reply

Asante kwa salamu. Natoweka sasa kwa wiki kadhaa - nitarudi baadaye. --87.175.184.142 13:07, 23 Julai 2007 (UTC)Reply

Makala Mpya hariri

Habari Ndugu Joel, Ni kuhusu makala ya Leonardo da Vinci: ndugu yangu wewe una muda mrefu sana katika uchangiaji wa makala katika Wikipedia ya Kiswahili vipi tena uandikie makala kwa ufupi tena bila hata kuweka ile alama ya kuonyesha makala inahitaji iendelezwe (Mbegu). mwanzo nilifikiri wewe ni mgeni kumbe upo miaka mingi au ndo mchanganyo?. lakini tayari nimesha fanya marekebisho kadha wa kadha unaweza kuitembelea kwa sasa ukaangalia na ukaongeza mambo mengine. sina mengi wako katika ujenzi wa Wikipedia --Muddyb Blast Producer 06:33, 26 Septemba 2007 (UTC)Reply

Habari Ndugu Joel, Nashukuru kwa kunifamisha nini kilitokea kuhusiana na makala ile. Na pia tuongeze mkazo kama unavyosema ila inaonekana siku hizi uhadimu kidogo au ndo majukumu?. Pia naona mzee kipala ametoa pongezi kwa kufikia makala 6'000, kwa watu walioshriki kuandika makala natumai wewe ni mmoja wao, ni hayo tu sina mengi wako katika ujenzi wa wikipedia --Muddyb Blast Producer 05:34, 27 Septemba 2007 (UTC)Reply

Kimya Mno hariri

Salam nyingi Nd. Joel, Kaka ni mda sasa sijakuona vipi tena au ndio majukumu!!--Mwanaharakati 07:05, 30 Oktoba 2007 (UTC)Reply

Shirikiana na Wiki Loves Love 2019 kuuweka utamaduni wako kwenye nyaraka na ushinde zawadi za kusisimua! hariri

 

⧼Tafadhali-tafsiri⧽

Afrika ina matamasha mazuri, sherehe na maadhimisho ya upendo. Tunahitaji msaada wako kwaajili ya kuweka kumbu kumbu hizi! Hizo ni msingi wa utamaduni wa Afrika na ili kuhakikisha mfumo huo wa maisha uliofuatwa na mababu zetu unabaki miongoni mwetu, tunahitaji kuwa nao mtandaoni ili kuhakikisha umehifadhiwa. Waunge mkono Wiki Loves Love kwa dhumuni la kuhifadhi kumbu kumbu na kusambaza namna upendo ulivyo oneshwa kwa tamaduni zote kupitia mila mbali mbali, sherehe na matamasha na upate nafasi ya kushinda zawadi ya kusisimua!! Wakati unapo pakia, tafadhali ongeza nchi yako katika kanuni za Wikimedia. Kama unataka kuandaa kwenye tovuti ya matukio ya Wiki Loves Love,wasiliana na our international team! Kwa taarifa zaidi, angalia ukurasa wetu wa mradi project page kwenye kanuni za Wikimedia.

Kuna zawadi zaidi za kunyakua. Tunatumaini kukuona unasambaza upendo na Wiki Loves Love Februari hii!

Fikiria...Kiasi cha upendo wote!

Wiki Loves Love team 07:34, 4 Februari 2019 (UTC)

Kisiwa cha Toten hariri

Asante kwa picha nzuri. Kama umeingia katika maktaba Tanga je ulikuta habari zozote kuhusu chanzo cha makaburi? Sidhani ya kwamba maelezo katika makala ni swa. Hakuna sababu ya kutenga watu wenye malaria maana si ugonjwa wa kuambukizwa. Hakika hii ilijulikana hata wakati ule. Baada ya kuona picha napata swali kama labda ilikuwa makaburi ya kawaida ya Wajerumani walioamua kuyaanzisha pale kisiwani kwa sababu kiko karibu na kitovu cha mji. Unaonaje? Kipala (majadiliano) 23:02, 25 Februari 2019 (UTC)Reply