Majadiliano ya mtumiaji:Kipala/makala 10000
Kipala salaam. Maoni yangu ni kwamba orodha ya viumbehai haina vidahizo vya kutosha kutoka Afrika. Nafikiri kwamba tungeongeza vidahizo vingine na kuondoa vingine. ChriKo (majadiliano) 19:45, 31 Mei 2020 (UTC)
Basi tuangalie namna ya nyongeza. Kimsingi nimeleta hapa tu orodha ya Meta jinsi ilivyo maana inasaidia kutambua mapengo. Pia nina "hobby" kidogo kusukuma swwiki juu zaidi katika takwimu za wikipedia. Ni kweli kwamba habari za Afrika ni chache. Mimi napendekeza tuongeze lemma kwa kuweka alama ya *kabla ya istilahi. Kipala (majadiliano) 15:14, 1 Juni 2020 (UTC)
- Sawasawa, tufanye hivyo. ChriKo (majadiliano) 16:06, 1 Juni 2020 (UTC)
- Mimi naona tuongeze bila kupunguza. Pia kulikuwa na toleo fulani, lililokuwa limeshaongezewa makala za Kiafrika zaidi. Ni hili: Wikipedia:Makala za msingi 1000 - orodha ya awali iliyopanuliwa. Amani kwenu! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:52, 2 Juni 2020 (UTC)
Kupanuliwa
haririNinaona hapa ni mahali pazuri pa kuendeleza badala ya kuanza upya kila siku. Ni kweli kila mmoja ana hiyari yake ya kuunda makala apendezo lakini kuboresha kile kinachotakikana katika kila Wikipedia ni bora zaidi. Nitarudi hapa! Muddyb Mwanaharakati Longa 19:26, 7 Julai 2024 (UTC)