Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Mr Accountable (majadiliano) 15:05, 24 Novemba 2009 (UTC)Reply

Kompyuta hariri

Naomba radhi kwamba palikuwapo na kutoelewana kuhusu ni makal gani yaliyokuwa yakiandikwa. Makala yaliyoandikwa ni Tarakilishi ambayo kwa hakika ni mbegu. Makala niliyotafsiri yalikuwa yale ya Kiingereza ya Computer, si ile mbegu ya Kiswahili. Kwa bahati mbaya, sikuona kama makala yale ya tarakilishi yalikuwa yameandikwa. Nadhani badala ya kuyafuta yote, labda ungejadili kuhusu namna ya kuyaunganisha ila sitaki kukakawana vile. Iwapo hayakuwa ya maana pia ni vizuri kwamba yaondolewe. Wakati mwema.

Nimerejesha mabadiliko uliyofanya katika makala husika. Kuandika juu ya kazi ya wengine bila majadiliano si utaratibu wetu. (linganisha pia masharti ya mashindano).

 
Onyo dhidi ya kuandika juu ya kazi ya wengine bila taarifa

Ulichangia makala katika wikipedia hii. Asante sana! Kwa bahati mbaya ulichagua kichwa kilichokuwepo tayari. Ukitumia google-translate labda hujatambua ya kwamba uliweka tafsiri yako juu ya makala iliyopo tayari.

Ni sawa kabisa ukibadilisha makala, au kuongeza mambo ndani yake.

Mara chache ni afadhali kufuta yote. Ila tu hapa kwenye wikipedia tunajadiliana kabla ya kufuta kazi ya wengine. Kuna ukurasa wa majadiliano unapoweza kutaja sababu kwa nini makala jinsi ilivyo si nzuri halafu subiri siku 2 hadi kufanya mabadiliko makubwa. Unaweza pia kiuangalia historia ya makala na kumwandikia mchangiaji aliyetangulia moja kwa moja.

Haikubaliki kufuta kazi ya wengine kimya-kimya. Hata kama hujakusudia kufanya hivyo tulilazimishwa kufuta kazi yako na kurejesha hali ya awali. Uko huru kuchukua sehemu za maandishi yako na kupeleka kama nyongeza katika makala iliyopo.

--Kipala (majadiliano) 08:52, 17 Desemba 2009 (UTC)Reply