Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Kipala (majadiliano) 08:37, 18 Desemba 2015 (UTC)Reply


Usiendelee vile!

hariri

Rafiki naona umeshika hoja ya kuingiza hapa makala kutoka ukurasa wa trt Swahili kama makala. Unatumia njia ya kopi-paste. Naona huna nia mbaya lakini hii haikubaliki, inaweza kusababisha matatizo ya kisheria. Pamoja na hayo si njia tunayopenda na kukubali hapa wikipedia. Michango yako yote ni kunakili tu na kuweka hapa. Kwa hiyo itafutwa yote.

Ukipenda kuchangia kwa maana basi chukua makala kuhusu Leo katika historia kabla haijafutwa na ingiza habari za maana kwenye makala ya 23 Januari. Vivyo hivyo unaweza kutumia habari kutoka makala nyingine na kuunda makala yenye maana kwa mfano kuhusu Yunus Emre. Pia ungeweza kutuia habari za makala na kuongeza makala zilizopo kwa mfano kuhusu Bosnia na Herzegovina. Hapo unapaswa kuangalia msimamo wa kutopendelea upande. Yaani pale ambako makala yanarudia tu msimamo wa serikali ya Uturuki kuhusu jambo usionyeshe hii kama ukweli kamili, unaweza kuitaja kama msimamo wa Kituruki. Kipala (majadiliano) 20:13, 25 Januari 2016 (UTC)Reply

Pole, Ndg TrtSwahili, nimeshafuta makala ya Leo katika historia, lakini unaweza kuangilia jinsi nilivyoingiza habari zake katika makala ya 23 Januari. Naomba ufuate mashauri ya Ndg Kipala. Asante. --Baba Tabita (majadiliano) 20:22, 25 Januari 2016 (UTC)Reply