Makanikaumeme
Makanikaumeme (kwa Kiingereza: electromechanics) ni tawi la uhandisi linalounganisha elimu ya umeme na umakanika. Umuhimu wake ni hasa katika matumizi ya nguvu ya umeme kwa kuendesha mashine na vifaa vya kimakanika.

Rilei yenye sehemu za kiumeme na kimakanika
Vifaa vya aina hiyo ni vingi, kuanzia mkono wa saa unaosogezwa kwa nguvu ya umeme hadi mota ya umeme inayoendesha gari, lakini viendeshi diksi au pinta katika teknolojia ya kompyuta.
MarejeoEdit
- Omari M. Kiputuputi, Kamusi Sanifu ya Kompyuta, TATAKI, Dar es Salaam 2011, ISBN 9789987531127