"Make It Rain" ni wimbo pekee kutoka katika albamu ya Fat Joe ya Me, Myself & I. Wimbo umeshirikisha Lil Wayne, ambaye humu kaimba kiitikio tu (lakini pia ameshiriki kuimba katika remix yake). Wimbo umetayarishwa na mtayarishaji machachari - Scott Storch. Wimbo umebahatika kushika nafasi ya 13 katika chati za muziki wa hip hop kwa Billboard Hot 100. Wimbo pia umechukuliwa kuwa kama na athari za mtindo wa maisha ya msanii wa zamani wa muziki huo Bw. Pacman Jones.

“Make It Rain”
“Make It Rain” cover
Kasha ya single wa Fat Joe
Single ya Fat Joe na Lil Wayne
kutoka katika albamu ya Me, Myself & I
Imetolewa Oktoba 2006
Muundo CD single
Imerekodiwa 2006
Aina Hip Hop
Urefu 4:11
Studio Terror Squad
Mtunzi J. Cartagena, S. Storch, D. Carter
Mtayarishaji Scott Storch
Mwenendo wa za Fat Joe
"Get It Poppin"
(akimshirikisha Nelly)
(2005)
"Make It Rain"
(2006)
"We Takin' Over"
(2007)
Mwenendo wa za Lil' Wayne
"Stuntin' Like My Daddy"
(2006)
"Make It Rain"
(2006)
"You" Lloyd akimshirikisha Lil Wayne)
(2006)

Video yake

hariri

Waliouza sura katika video hii ya make it rain alikuwa DJ Khaled, Cool na Dre, Scott Storch, Birdman, Diddy, Rick Ross, Oliver Coats, Triple C, Hennessi, na Young Money. Video iliongozwa na Bw. Roboto na VinCock na kutayarishwa na Nicole Acacio kwa kampuni ya utengenezaji wa filamu ya Robot Films.

Chati za (2007) Nafasi
Iliyoshika
U.S. Billboard Hot 100 13
U.S. Billboard Hot 100 Airplay 14
U.S. Billboard Hot Digital Songs 13
U.S. Billboard Hot RingMasters 4
U.S. Billboard Nyimbo kali za R&B/Hip-Hop 6
U.S. Billboard Nyimbo kali za Rap 2
U.S. Billboard Pop 100 26
United World Chart 37
MTV Base chart UK 8
Deutsche Black Charts 11
New Zealand Top 50 14

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri