Mamie Geneva Doud Eisenhower (14 Novemba 1896 - 1 Novemba 1979) alikuwa mke wa Rais-Jenerali wa zamani wa Marekani Bw. Dwight D. Eisenhower. Alianza kuwa Mwanamke wa Kwanza wa Marekani kuanzia mwaka 1953 hadi 1961. Mamie na Eisenhower walioana mnamo mwezi Julai ya mwaka wa 1916.

Mamie Eisenhower akiwa katika Ikulu ya Marekani.

Mamie alizaliwa mjini Boone, Iowa. Alikuwa mtoto wa mzee John Sheldon Doud. Babake na Mamie alikuwa tajiri wa kutosha, kwakuwa alikuwa anamiliki kiwanda cha kusindika nyama za kopo. Kuna kipindi, familia ya mzee Doud iliishi kidogo mjini Pueblo, Colorado.

Kisha Familia ikahamia na kuweka makazi yake rasmi katika mji wa Denver, Colorado. Wakiwa huko, Mamie na ndugu zake wengine wa kike watatu walikulia huko wakiwa katika mazingira ya mjumba mkubwa kabisa usio na kifani. Na nyumba ilikuwa na wahudumu wengi kupita kiasi.

Ilipofika mnamo mwaka wa 1915 Mamie alkakutana na Bw. Dwight D. Eisenhower. Na kwa kipindi hicho Bw. Eisenhower alikuwa na cheo cha Luteni masaidizi katika Jeshi. Mwaka uliofuatia katika siku ya wapendanao duniani, wawili hao wakavishana pete ya uchumba. Na ilivyofika tar. 1 Julai ya mwaka wa 1916 wakajaaliwa kuoana.

Viungo vya nje

hariri



Orodha ya Wake wa Marais wa Marekani  
M. Washington · A. Adams · M. Jefferson Randolph · D. Madison · E. Monroe · L. Adams · E. Donelson · S. Jackson · A. Van Buren · A. Harrison · J. Harrison · L. Tyler · P. Tyler · J. Tyler · S. Polk · M. Taylor · A. Fillmore · J. Pierce · H. Lane · M. Lincoln · E. Johnson · J. Grant · L. Hayes · L. Garfield · M. McElroy · R. Cleveland · F. Cleveland · C. Harrison · M. McKee · F. Cleveland · I. McKinley · Edith Roosevelt · H. Taft · Ellen Wilson · Edith Wilson · F. Harding · G. Coolidge · L. Hoover · E. Roosevelt · B. Truman · M. Eisenhower · J. Kennedy · C. Johnson · P. Nixon · B. Ford · R. Carter · N. Reagan · B. Bush · H. Clinton · L. Bush · M. Obama