Manassa Danioko

Mwanasheria wa Mali

Diakité Manassa Danioko (alizaliwa Kadiolo, Mali, 19 Januari 1945) ni mwanasheria na mwanadiplomasia wa Mali. Alihudumu kama rais wa mahakama ya kikatiba ya nchi hiyo kutoka mwaka 2015 hadi 2020.[1]

Elimu na kazi hariri

Danioko alipata shahada mwaka 1966[1] akapokea shahada ya uzamili katika sheria kutoka shule ya kitaifa ya utawala mwaka 1970.[2]

Dianoko aliwahi kuwa rais wa mahakama ya kazi au Ségou kuanzia 1970 hadi 1971, na alishiriki katika mfululizo wa mafunzo ya mahakama nchini Ufaransa kuanzia Oktoba 1971.[1] Kuanzia 1972 hadi 1978, alikuwa naibu mwendesha mashtaka katika mahakama ya mwanzo.[2] Alikuwa wakili mkuu wa mahakama ya rufaa ya Bamako kuanzia 1979 hadi 1981,[1] baraza kuu la mahakama kutoka 1979 hadi 1988, na mshauri wa mahakama maalum ya usalama wa nchi kutoka 1983 hadi 1988.[2]

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "Pioneer African Women in Law". African Women in Law (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-12-23. 
  2. 2.0 2.1 2.2 "Manassa Danioko". African Women in Law (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-12-23.