María Abella

Mwandishi wa Uruguay

María Abella de Ramírez (28 Septemba 18635 Agosti 1926) alikuwa mwanaharakati wa haki za wanawake wa nchini Uruguay, aliyejulikana kwa kuanzisha vikundi vya wanawake wa Uruguay na Argentina mnamo miaka ya 1900.

Abella alichapisha jarida la We Women(Nosotras), na alikuwa mchangiaji wa jarida la National Feminist League journal.

Maisha hariri

Maria Abella Alijihusisha na harakati za freethinking movement nchini Argentina, mwaka 1903 Abella aliunga mkono kuundwa kwa kituo cha utetezi wa haki za wanawake ili kuwezesha majadiliano, baadaye akielezea "mpango wake wa chini wa uthibitisho wa wanawake" katika Kongamano la Freethinker la 1906, akibishania fursa sawa na kulipa kwa wanawake. Pia alipigania haki za talaka za wanawake huku akikabiliwa na upinzani kutoka kwa Kanisa Katoliki la Roma. Hata vikundi vinavyounga mkono talaka viliacha sauti na mwili wa kike; mnamo 1905, mswada uliopendekezwa wa Oneto y Viana ulihalalisha talaka, lakini ulithibitisha sababu kama uzinzi wa kike katika visa vyote. [1] Abella pia alisema kuwa serikali haikuwa na haki ya kudhibiti biashara ya ngono, ambayo alitangaza katika mkutano wa 1906:

Mnamo mwaka 1909, Abella alianzisha National League of Women Freethinkers akiwa na Dk. Julieta Lanteri, na mwaka 1910 Abella alianzisha National Women's League huko La Plata, Argentina . Shirika hili liliunga mkono upigaji kura wa wanawake, na liliunganishwa na International Woman Suffrage Alliance.

Vyanzo hariri

Marejeo hariri

  1. Lavrin, Asunción (1998). Women, Feminism and Social Change in Argentina, Chile, and Uruguay, 1890 - 1940. University of Nebraska Press. p. 253. ISBN 978-0-8032-2897-9. 
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu María Abella kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.