Maracaibo (tamka ma-ra-ka-i-bo) ni mji mkubwa wa pili nchini Venezuela; ni jiji lenye wakazi 2,658,355[1] ilhali rundiko la mji huwa na watu 5,278,448 (mwaka 2010).[2] Maracaibo uko upande wa magharibi wa mfereji mpana unaounganisha Ziwa Maracaibo na Bahari Karibi.

Maracaibo
Kitovu cha jiji la Maracaibo
Nchi Venezuela
Jimbo / Mkoa Zulia
Manisipaa Maracaibo
Anwani ya kijiografia 10°38′N 71°38′W / 10.633°N 71.633°W / 10.633; -71.633
Eneo km2 1,393
Wakazi 2,658,355

Maracaibo hutazamwa kuwa kitovu cha uchumi cha magharibi mwa Venezuela. Kuna tasnia muhimu inayotumia mafuta ya petroli yanayopatikana kwenye mwambao wa Ziwa Maracaibo. Ilikuwa mji wa kwanza wa nchi uliokuwa na umeme.

Wakazi asilia walikuwa Maindio wa makabila ya Waarawak na Wakaribi. Wajerumani na Wahispania walianzisha mji mara kadhaa lakini ulibomolewa tena na Maindio hadi kuwa na makazi ya kudumu kuanzia mnamo 1574. Mafuta yaligunduliwa mnamo mwaka 1917 na kuanzia mwaka huu idadi ya wakazi iliongezeka sana kutokana na watu wengi waliohamia eneo la Macaraibo wakitafuta ajira.

Maracaibo huwa na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa La Chinita. Daraja refu la mita 8,678 linaunganisha Maracaibo na sehemu nyingine za Venezuela.

Marejeo

hariri
  1. [1] https://web.archive.org/web/20091114075110/http://www.ine.gov.ve/seccion/poblacion/magnitudestructura/Trabajo.asp?CodigoEstado=24&TipoPublicacion=Proyecciones&AreaDePublicacion=poblacion&AnoBaseCenso=2001&CodigoCuadro=Cuadro_06&ControlHref=14&strHref=MunicipioMaracaibo&strMunicipioX=Municipio$Maracaibo |date=November 14, 2009
  2. [2] https://web.archive.org/web/20091114000814/http://www.ine.gov.ve/seccion/poblacion/magnitudestructura/MenuMagnitud.asp?Codigo_Estado=24&Publicacion=Proyecciones&AnoBaseCenso=2001&AreaDepublicacion=poblacion&seccion=2&nedo=24%23 date=November 14, 2009
  Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Maracaibo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.