Maulana Ron Karenga
Maulana Ron Karenga (anajulikana pia kama Ron Everett na Maulana Karenga; alizaliwa na jina Ronald McKinley Everett 14 Julai 1941) ni mwandishi Mmarekani mweusi na mwalimu wa chuo anayejulikana zaidi kama mwanzilishi wa sherehe ya Kwanzaa tangu mwaka 1966.
Maulana Ron Karenga | |
Amezaliwa | Ronald McKinley Everett 14 Julai 1941 Maryland, Marekani |
---|---|
Nchi | Marekani |
Kazi yake | Profesa Mwandishi |
Ndoa | Brenda Lorraine "Haiba" Karenga (Talaka) Tiamoyo Karenga (1970-hadi leo) |
Tovuti | http://www.maulanakarenga.org/ |
Karenga alikuwa mwanafunzi wakati wa miaka ya 1960 kwenye chuo kikuu cha Kalifornia mjini Los Angeles. Baada ya kukutana na Malcolm X akajiunga na vikundi vya "Black Power". Wakati ule alianza kubadilisha jina lake akajiita mwanzoni Ron Ndabezitha Everett-Karenga baadaye alianza kutumia jina la "Maulana". Tangu 1965 aliongoza kundi lililoitwa "Us". Alishindana na Black Panthers kuhusu uongozi kati ya wanafunzi mapamabano yakawa vikali hadi kutokea kwa mapigano ya silaha ambamo wana Black Panther 2 waliuawa na Wana-Us tar. 17 Januari 1969.
Karenga aliendelea kuongoza kundi hadi kukamatwa 1971 na kufikishwa kotini kwa mashtaki ya kutesa wakinamama 2 wa kundi lake aliwafunga mikono na miguu akawapiga na mmoja akamchoma mdomo na kuvunja mguu. Alipewa adhabu ya jela akakaa ndani kwa muda wa miaka 4 hadi 1975.
Alipotoka jela aliendelea masomo yake akafikia stashada ya dokta.
Karenga alianzisha Kwanzaa kama sherehe ya Wamarekani weusi alioona ambao alitaka wawe na sikukuu tofauti na Krismasi aliyoona kama sikukuu ya Kizungu.
Karenga alijitahidi kupamba sherehe ya Kwanzaa na desturi alizoelewa ni za Kiafrika pamoja na maneno na majina mengi ya Kiswahili au ya kufanana na Kiswahili.
Tangu miaka ya 1980 alikuwa mwalimu wa chuoni.
References
haririViungo vya Nje
hariri- The Organization Us
- A Post-Obama Kwanzaa -- By Dr. Michael Eric Dyson, 23 Desemba 2008.
- Biography of Dr. Ron "Maulana" Karenga. Ilihifadhiwa 19 Mei 2003 kwenye Wayback Machine.
- Interview with Dr. Karenga, PBS Public Broadcasting Service and WGBH/Frontline
- The Story of Kwanzaa by Laurence Scholer, The Dartmouth Review, 15 Januari 2001, a criticism of Karenga and the holiday
- 500 Years Later The Film Site
- IMDB Profile
- The Official Kwanzaa Web site - Dr. Maulana Karenga Ilihifadhiwa 24 Septemba 2009 kwenye Wayback Machine.
- Scot Brown, Fighting for US: Maulana Karenga, the US Organization, and Black Cultural Nationalism, NYU Press, New York, 2003.
- Federal Bureau of Investigation (FBI) Monograph about US, April, 1968
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Maulana Ron Karenga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |