Mbaazi
(Cajanus cajan)
Mbaazi
Mbaazi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Fabales (Mimea kama mharagwe)
Familia: Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Nusufamilia: Faboideae (Mimea inayofanana na mharagwe)
Jenasi: Cajanus
Spishi: C. cajan
(L.) Huth

Mbaazi (Cajanus cajan) ni mmea wa mazao wa nusufamilia Faboideae katika familia Fabaceae. Mbegu zake huitwa mbaazi pia. Mmea huu hukuzwa sana katika maeneo makavu ya tropiki na nusutropiki.

Zao hili hustahimili hali ya ukame[1] na utunzaji wake hautumii gharama kubwa wala muda mwingi kulihudumia.

Kwenye nchi za Afrika Mashariki mbegu za mmea huu au zao hili hutumika kama mboga[2] hasa kwenye chakula kama vile wali na ugali.

Tanbihi

hariri
  1. Justdiggit. "Ukame na mmomonyoko wa udongo". Justdiggit. Iliwekwa mnamo 2024-06-05.
  2. "Kilimo cha mboga, matunda kinavyozibeba familia nyingi". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2023-01-24. Iliwekwa mnamo 2024-06-05.
  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mbaazi (mmea) kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.