Mbofu
Mbofu wa Malawi (Bagrus meridionalis)
Mbofu wa Malawi (Bagrus meridionalis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Siluriformes (Samaki kama kambale)
Familia: Bagridae (Samaki walio na mnasaba na mbofu)
Bleeker, 1858
Jenasi: Bagrus
Bosc, 1816
Ngazi za chini

Spishi 11:

Mbofu au mbuvu ni samaki wa maji baridi wa jenasi Bagrus katika familia Bagridae na oda Siluriformes ambao wanatokea Afrika tu. Bagrus tucumanus ameelezwa kutoka Argentina lakini huenda jina hili ni kisawe cha Luciopimelodus pati.

Maelezo

hariri

Miongoni mwa samaki kama kambale mbofu ni wakubwa, hadi m 1.5. Mwili ni uchi kabisa yaani hawana magamba. Pezimgongo linatanguliwa na mwiba. Pezi lenye shahamu liko na linaweza kuwa na msingi mrefu kiasi katika spishi fulani. Miiba wa mapeziubavu inaweza kuwa na meno. Samaki hawa wana jozi nne za sharubu ambazo zimefunikwa kwa tabaka la epitelio lenye matumba mengi ya uonjaji.

Spishi za Afrika

hariri

Marejeo

hariri
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mbofu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.