Mbuga wa safari (ing.: safari park) ni aina ya zoo penye wanyama wa pori lakini yenye eneo kubwa ambako watu wanaweza kutembea kwa magari kati ya wanyama walio ndani ya vifungo vyao. Hii ni tofauti na zoo za kawaida ambako watalii wanatembea kwenye njia kati ya vifungo vya wanyama.

Twiga katika mbuga wa safari nchini Uholanzi
Kifaru katika mbuga wa safari San Diego, Kalifornia, Marekani

Sawa na zoo wanyama wanaoweza kuwindana au kupigana hawako pamoja ndani kifungo kimoja. Lakini maeneo ni makubwa zaidi kuliko zoo ya kawaida.

Mbuga za aina hii zilianzishwa huko Marekani mnamo mwaka 1953 katika jimbo la Florida ambako simba 12 waliwekwa ndani ya fensi katika eneo la hektari 1 na watalii waliweza kupita kwa gari.

1966 ikafuata mbuga mwingine huko Longleat, Uingereza ambako eneo la hektari 40 (ekari 99) lilitengwa kwa kusudi hili. Katika miaka ya 1970 mbuga mbalimbali zilijengwa Ulaya na Marekani na pia Asia zenye maeneo ya zaidi ya hektari 100 yaani kilometa ya mraba 1. Mahali pachache kama vile San Diego, Marekani (7.3 km²) na Cox Bazar, Bangla Desh (9.6 km²) kuna mbuga kubwa zaidi. Hizi zote ni ndogo kabisa kuliko mbuga za wanyama katika Afrika penye maeneo ya kilomita za mraba makumi hadi maelfu na hapa wanyama hawatengwi. Mbuga za Afrika zinalenga kuhifadhi wanyamapori katika mazingira asilia lakini mbuga za safari zinataka kuonyesha wanyamapori katika mazingira isiyo ya kiasili tena kwa makusudi ya kibiashara pamoja na kielimu na kiburudani.