Mbofu
(Elekezwa kutoka Mbuvu)
Mbofu | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mbofu wa Malawi (Bagrus meridionalis)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 11:
|
Mbofu au mbuvu ni samaki wa maji baridi wa jenasi Bagrus katika familia Bagridae na oda Siluriformes ambao wanatokea Afrika tu. Bagrus tucumanus ameelezwa kutoka Argentina lakini huenda jina hili ni kisawe cha Luciopimelodus pati.
Maelezo
haririMiongoni mwa samaki kama kambale mbofu ni wakubwa, hadi m 1.5. Mwili ni uchi kabisa yaani hawana magamba. Pezimgongo linatanguliwa na mwiba. Pezi lenye shahamu liko na linaweza kuwa na msingi mrefu kiasi katika spishi fulani. Miiba wa mapeziubavu inaweza kuwa na meno. Samaki hawa wana jozi nne za sharubu ambazo zimefunikwa kwa tabaka la epitelio lenye matumba mengi ya uonjaji.
Spishi za Afrika
hariri- Bagrus bajad, Mbofu Bayadi (Bayad)
- Bagrus caeruleus, Mbofu Buluu (Blue catfish)
- Bagrus degeni, Mbofu wa Viktoria (Lake Victoria bagrus)
- Bagrus docmak, Kibogobogo au Semutundu (Semutundu)
- Bagrus filamentosus, Mbofu wa Mto Nijeri (Niger River bagrus)
- Bagrus lubosicus, Mbofu wa Mto Lubosi (Lubosi River bagrus)
- Bagrus meridionalis, Mbofu wa Malawi (Kampango au Kampoyo)
- Bagrus orientalis, Kitoga au Mbofu Mashariki (Eastern bagrus)
- Bagrus tucumanus, Mbofu wa Argentina (Argentinian bagrus) - labda kisawe cha Luciopimelodus pati
- Bagrus ubangensis, Mbofu wa Kongo (Congo bagrus)
- Bagrus urostigma, Mbofu wa Mto Juba (Somalia catfish)
Marejeo
hariri- Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
- Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mbofu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |