Cherimiyo
(Elekezwa kutoka Megabyas)
Cherimiyo | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Cherimiyo rangi-mbili
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Cherimiyo ni ndege wadogo wa jenasi Bias na Megabyas katika familia Platysteiridae wanaotokea Afrika kusini kwa Sahara. Zamani waliainishwa katika familia Muscicapidae. Labda Bias ina mnasaba zaidi na milali (Prionopidae).
Kila jenasi ina spishi moja tu. Dume la spishi zote mbili ni mweusi juu na mweupe chini, lakini cherimiyo-mbwigu ana kishungi na koo lake ni jeusi. Jike ni kahawia au kahawiachekundu. Cherimiyo hula wadudu na hulijenga tago lao kwa majani, uvumwani na utando wa buibui na kwa umbo wa kikombe katika mti au kichaka. Jike huyataga mayai 2-4.
Spishi
hariri- Bias musicus, Cherimiyo Rangi-mbili (Black-and-white Shrike-flycatcher)
- Megabyas flammulatus, Cherimiyo-mbwigu (African Shrike-flycatcher)
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Cherimiyo kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |