Nyoka Laini
(Elekezwa kutoka Meizodon)
Nyoka laini | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 5:
|
Nyoka laini ni nyoka wa jenasi Meizodon katika familia Colubridae. Wamepewa jina hili kwa sababu ya ngozi yao laini.
Nyoka hawa ni wafupi na wembamba, sm 80 kwa kipeo lakini sm 30-60 kwa kawaida. Rangi ya wapevu ni kijivu au kahawia lakini nyoka laini kichwa-cheusi ni mwekundu au pinki wenye kichwa cheusi na shingo yenye mkufu mweusi. Wachanga ni kijivu au hudhurungi na kwa kawaida wana mabaka meusi angalau kichwani au kwa nusu ya mbele ya mwili pia.
Nyoka laini hukiakia mchana na hula mijusi, vyura na wagugunaji wadogo.
Nyoka hawa hawana sumu na wanaweza kukamatwa bila shida kwa sababu hawang'ati kwa kawaida.
Spishi
hariri- Meizodon coronatus, Nyoka-taji Magharibi (Western crowned snake)
- Meizodon krameri, Nyoka Laini wa Tana (Tana Delta smooth snake)
- Meizodon plumbiceps, Nyoka Laini Kichwa-cheusi (Black-headed smooth snake)
- Meizodon regularis, Nyoka-taji Mashariki (Eastern crowned snake)
- Meizodon semiornatus, Nyoka Laini Nakshi (Semi-ornate snake)
Marejeo
hariri- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyoka Laini kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |