Metali alikali

(Elekezwa kutoka Metali ya alkali)

Metali alikali (kwa Kiingereza: alkali metal) ni elementi za kundi la kwanza katika mfumo radidia hasa lithi, natiri, kali, rubidi, caesi na fransi. Hidrojeni ni pia elementi ya kundi la kwanza lakini kwa kawaida haionyeshi tabia za metali alikali.

Zote ni metali zinazong'aa kwa rangi ya kifedha-nyeupe zenye elektroni moja tu katika mzingo elektroni wa nje, yaani zina valensi moja.

Kwa sababu hiyo humenyuka haraka na dutu nyingi hazipatikani kwa umbo safi kiasili. Kama zimesafishwa katika maabara zinatunzwa katika angahewa ya gesi adimu au ndani ya mafuta bila kugusana na oksijeni.

Kati ya metali ni laina zakatwa kwa kisu. Densiti husianifu ni ndogo.

Uhusiano kati ya uzani atomia na tabia mbalimbali

hariri

Tabia mbalimbali hubadilika pamoja na kuongezeka kwa uzani atomia: elektrohasi yapungua, mmemenyuko huongezeka na viwango vya kuchemka au kuyeyuka hupungua.

Metali alikali Uzani atomia Kiwango cha kuyeyuka (K) Kiwango cha kuchemka (K) Elektrohasi (Pauling)
Lithi 6.941 453.69 1615 0.98
Natiri 22.990 370.87 1156 0.93
Kali 39.098 336.53 1032 0.82
Rubidi 85.468 312.46 961 0.82
Caesi 132.905 301.59 944 0.79
Fransi (223) ? 295 ? 950 0.7


  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Metali alikali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.