Kisu (maana yake "msu mdogo"; wingi: visu) ni kifaa cha kukata chenye bapa ambalo ni kali angalau upande moja. Kwa kawaida kuna sehemu mbili: bapa kali na shikilio. Siku hizi bapa imetengenezwa kwa metali na shikilio la ubao au plastiki.

Kisu cha jikoni
Visu vya mawe (zama za mawe ya mwisho)

Historia ya kisu

hariri

Visu vimepatikana tangu miaka lakhi: ni kati ya vifaa vya kwanza vilivyotengenzwa na binadamu tangu zama za mawe. Chanzo kilikuwa katika mawe yaliyochongwa ili kupata kona kali kwa shughuli za kukatakata.

Katika mwendo wa zama za mawe uwezo wa binadamu uliongezeka na shoka za mkononi za awali ziliweza kutengenezwa nyembamba zaidi hadi kufikia bapa la jiwe kamili.

Tangu kupatikana kwa bronzi visu vilitengenezwa zaidi kwa metali. Leo hii visu vingi vina bapa ya feleji. Siku hizi kua pia visu vya bapa za ufinyanzi wa seramiki.

 
Kisu mashuhuri cha jeshi la Uswisi kinaunganisha vifaa vingi ndani yake

Aina za visu

hariri
  • Visu vya jikoni: ni visu vinavyotumiwa na mpishi. Ni visu vikali vinavyofaa kukata haraka mboga na nyama itakayopikwa. Kuna visu vodogo pia visu virefu.
  • Visu vya meza: Visu hivi vinawekwa kando la sahani kwa kila mtu kwa matumizi ya kukata chakula mezani. Ilhali chakula kimeshapikwa tayari si muhimu ya kwamba visu hivi ni vikali sana.
  • Visu vya mwindaji ni visu vikubwa na vikali vinavyohitajika kukata ngozi ya wanyama na kupasua windo.
  • Visu vya mvuvi vinahitaji ncha kali maana vinatumwa kufungua na kusafisha samaki aliyekamatwa.
  • Visu vya mjenzi ni visu vya pekee kwa matumizi ya kukata vifaa vya ujenzi kama vile karatasi na mapipa ya plastiki na kadhalika
  • Visu vya mwanajeshi ni visu vinavyokusudiwa kama silaha
  • Visu vya mfukoni ni visu vinavyoweza kukunjwa na kutunzwa kwenye mfuko wa suruali bila hatari.

Kisu na sheria

hariri

Nchi malimbali huwa na sheria zinazopiga marufuku aina kadhaa za visu. Hapo kuna kanuni kuhusu urefu wa bapa ambayo mtu anaruhusiwa kubeba. Kanuni nyingine zinakataza visu ambavyo havionyeshi bapa hadi kubonyeza sehemu ya kisu na bapa inatokea kwa ghafla.