Mfiwi mafuta
(Lablab purpureus)
Mfiwi mafuta
Mfiwi mafuta
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Fabales (Mimea kama mharagwe)
Familia: Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Jenasi: Lablab
Spishi: L. purpureus
(L.) Sweet

Mfiwi mafuta au mnjahe (Lablab purpureus) ni jina la mmea katika familia Fabaceae. Mbegu zake huitwa fiwi mafuta au njahe (kutoka na Kikikuyu: njahĩ). Mfiwi mafuta ni mmea wa Afrika unaokuzwa mahali popote katika ukande wa tropiki siku hizi.