Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (kwa Kiingereza: Universal Communications Service Access Fund, kifupi: UCSAF) ni taasisi iliyoanzishwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusaidia kuboresha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini nchini.

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)
AinaShirika linalomilikiwa na serikali
Ilipoanzishwa1 Julai 2009
Makao MakuuDar es Salaam, Tanzania
Eneo linalohudumiwaTanzania
Watu wakuuBi. Justina Mashiba Mtendaji Mkuu
SektaMawasiliano
MmilikiJamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tovutiucsaf.go.tz

Taasisi hii ilianza tarehe 1 Julai mwaka wa 2009 kwa Sheria ya Bunge nambari 11 ya mwaka 2006 Sura ya 422. UCSAF ipo chini ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Historia

hariri

Mabadiliko ya sekta ya mawasiliano kuanzia miaka ya 1990 yaliingiza ushindani katika sekta ya mawasiliano. Katika kuongeza ushindani katika soko la mawasiliano lilijitokeza ombwe lilitokana na nguvu za ushindani kujikita kupeleka mawasiliano katika maeneo yenye mvuto wa kibiashara na kuyaacha maeneo ya vijijini na ya mijini yasio na mvuto wa kibiashara.

Mwaka 2006, sheria ya kuanzisha mfuko mahsusi kwa ajili ya mawasiliano ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusainiwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2007. Hata hivyo kanuni za kuanzisha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote zilisainiwa mwezi Aprili 2009.[1]

UCSAF imejielekeza katika kubaini maeneo ya miradi ya mawasiliano ambayo yanaweza kupata ruzuku serikalini kupitia mfuko huo, lengo ni kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na huduma za uhakika za mawasiliano iwe ni mawasiliano ya simu za mkononi,[2] utangazaji wa redio na televisheni,[3] huduma za posta au intaneti.

Tangu kuanza kazi kwa UCSAF kumekuwa na mafanikio mengi katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania, miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na asilimia 66 ya maeneo ya kijeografia kupata huduma za mawasiliano, asilimia 94 ya wananchi wanaweza kupata mawasiliano. Kabla ya kuanzishwa kwake, asilimia 80 ya Watanzania waliokuwa wanaishi vijijini walikabiliwa na changamoto za mawasiliano.[4]

Mfuko unatekeleza mradi wa kuiongezea uwezo minara iliyokuwa katika teknolojia ya 2G kwenda 3G kuongeza upatikanaji wa intaneti. Kwa upande wa kuboresha mawasiliano ya simu, mfuko umekuwa ukishirikiana na watoa huduma za mawasiliano kwa kutoa ruzuku ambayo inawawezesha watoa huduma kufikisha huduma katika maeneo yasiyo na mawasiliano ama yenye mawasiliano hafifu.[5]

Mfuko unatekeleza pia miradi mbalimbali ya kuboresha mawasiliano katika maeneo yaliyoko mipakani kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi.[6]

Agosti 18, 2017, UCSAF ilisaini mkataba na kampuni nne zinazotoa huduma za mawasiliano kusambaza mawasiliano ya simu kwa kujenga miundombinu maeneo ya vijijini. Kampuni zilizosaini mkataba huo ni Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Kampuni ya Vodacom Tanzania, Kampuni ya Viettel Tanzania (Halotel) na Kampuni ya MIC Tanzania (TIGO).[7][8]

Tanbihi

hariri
  1. Udahiliportal Editor 03 (2021-11-13). "Universal Communications Service Access Fund (UCAF)". UDAHILIPORTAL.COM (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-07-03. {{cite web}}: |author= has generic name (help)CS1 maint: numeric names: authors list (link)
  2. "UCSAF to connect 1,235 wards to mobile communication network". IPP Media. Iliwekwa mnamo 2022-06-30.
  3. "UCSAF kunufaisha vyombo vya mawasiliano". Mtanzania (kwa American English). 2021-05-19. Iliwekwa mnamo 2022-07-03.
  4. Daily News Reporter in Dodoma (2020-08-05). "Tanzania: Ucsaf Sets Ground to Improve FM Broadcasting". allAfrica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-07-03.
  5. Michael Malakata (2021-05-27). "Tanzania relies on UCSAF, policy to chase down connectivity target". ITWeb Africa (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-07-03.
  6. "UCSAF kuboresha mawasiliano Kagera". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2021-02-07. Iliwekwa mnamo 2022-07-03.
  7. "UCSAF wasaini makubaliano na Airtel kupeleka mawasiliano vijijini". Airtel. Iliwekwa mnamo 2022-06-30.
  8. "Tanzanian telcos ink UCSAF contract to improve rural access". https://www.telegeography.com. Iliwekwa mnamo 2022-06-30. {{cite web}}: External link in |work= (help)

Viungo vya nje

hariri