Tanzania Telecommunications Corporation (zamani: Tanzania Telecommunications Company Limited) mara nyingi huitwa kwa kifupi TTCL, ni kampuni kongwe na kubwa zaidi ya mawasiliano ya simu nchini Tanzania. Kampuni ilianza kufanya kazi kufuatia mgawanyiko wa lililokuwa shirika la serikali lililojulikana kama Shirika la Posta na Mawasiliano Tanzania (TP&TC) mwaka 1993. TTCL ilikuwa inamilikiwa kabisa na Serikali ya Tanzania mpaka ubinafsishaji wa kampuni ulipofanyika tarehe 23 Februari 2001.

Tanzania Telecommunications
Corporation
Ilipoanzishwa1993 (ilianza kazi tarehe 1 Januari 1994)
Makao MakuuExtelecoms House, Samora Avenue, Kisutu, Dar es Salaam, Tanzania
Eneo linalohudumiwaTanzania
Watu wakuuWaziri Kindamba, Mkurugenzi
BidhaaTTCL Broad band, TTCL Mobile, IP VPN, Prepaid Services, Postpaid Services, Rafiki Public Phone, Leased Circuits, Internet Bandwidth, Broadband and Wholesale Administrator
HudumaHuduma za Mawasiliano
Mapatoincrease TSh.93 billion/= (2013)[1]
Net incomeincrease TSh.16 billion/= (2013)[1]
Wafanyakazi1,600 (Feb 2016)
MmilikiJamhuri ya Muungano wa Tanzania
TovutiTovuti ya TTCL
Mhandisi akiwa kazini kwenye matengenezo katika kituo cha mitambo cha TTCL, Mtwara Tanzania

TTCL inaongozwa kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 1993. Kampuni hii ina leseni ya huduma za msingi za simu kwa Tanzania Bara na Zanzibar na hivyo inamiliki na kuendesha mtandao wa simu Tanzania Bara na Zanzibar. Kabla ya ujio wa kampuni za simu mwishoni mwa 1994, kampuni ilikuwa ikifurahia ukiritimba Tanzania Bara na Zanzibar, ambapo Zanzibar Telecoms Limited (Zantel) ilikuwa kampuni ya pili yenye leseni ya msingi ya mawasiliano ya simu. Kampuni imekuwa katika menejimenti kadhaa za pamoja kutokana na kuyumba kwake kifedha hapo awali na imepitia awamu kadhaa za mabadiliko.

Imekuwa ikifanya kazi na Huawei Technologies Co. Ltd kama mchuuzi wa miundombinu ya kampuni na Ericsson kama msambazaji wa kimkakati wa muda mrefu wa kampuni.[2]

Historia

hariri

Historia ya awali

hariri

Historia ya TTCL inaanzia kwa mtoa huduma wa mawasiliano wa Afrika ya Mashariki. Mnamo 1933, iliyokuwa Kampuni ya Posta na Telegrafu ya Afrika Mashariki ilishughulikia huduma za Posta, Telegrafu na Simu katika mataifa matatu ya Afrika Mashariki (Tanganyika, Kenya na Uganda). Mnamo 1951 serikali ya Uingereza ilibadilisha Kampuni ya Posta na Telegrafu ya Afrika Mashariki na kutunga Sheria ya Posta na Mawasiliano ya Simu ya Afrika Mashariki mwaka wa 1951 ili kuanzisha Utawala wa Posta na Mawasiliano ya Simu wa Afrika Mashariki.[3]

Mwaka 1967, baada ya mataifa hayo matatu kupata uhuru, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ilianzishwa na kuchukua nafasi ya Mamlaka ya Huduma za Pamoja za Afrika ya Mashariki. Baadaye, Shirika la Posta na Mawasiliano ya Simu la Afrika Mashariki (EAP&TC) lilianzishwa na kuchukua nafasi ya Utawala wa Posta na Mawasiliano ya Simu wa Afrika Mashariki. Hata hivyo, miaka kumi baadaye, kuvunjika kwa EAC mwaka 1977 kulilazimisha nchi wanachama wa EAC kuanzisha upya biashara zao za kitaifa za Posta, Telegrafu na Simu. Kwa hiyo, mwaka wa 1978 nchini Tanzania shirika la serikali lilianzishwa chini ya jina la Shirika la Posta na Simu Tanzania (TPTC).[4]

Mwaka wa 1993 serikali ya Tanzania ilipofanya marekebisho makubwa kwenye mashirika ya umma, sekta ya Mawasiliano iliwekwa huru. Hii ilisababisha kugawanyika kwa TPTC; TPTC iligawanyika katika taasisi tatu tofauti, ambazo ni Shirika la Posta Tanzania, Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), na Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC).

Ubinafsishaji

hariri

Kutokana na kuongezeka kwa ushindani wa ndani na usimamizi mbovu serikali iliamua kubinafsisha kampuni. Ubinafsishaji wa sehemu ya TTCL ulianza tarehe 23 Februari 2001, ambapo kampuni ya Celtel International (iliyokuwa ikiitwa MSI Cellular) yenye makao yake makuu mjini Amsterdam, Uholanzi, pamoja na kampuni ya Kijerumani ya Detecon, zilipata hisa 35% kutoka Serikali ya Tanzania. Muungano huo ulichukua udhibiti wa Bodi na Menejimenti ya TTCL. Kuanzia tarehe 23 Februari 2001 na kuendelea, ulikuwa na kura ya turufu juu ya maamuzi makuu ya Bodi ya Wakurugenzi, haki ya kuteua menejimenti kuu, kuweka mpango wa biashara wa mwaka na kudhibiti maamuzi yote ya matumizi ya mtaji.[5] Mnamo Agosti 2005, TTCL ilijiondoa katika usimamizi wa pamoja, Serikali ya Tanzania na Celtel International zilitia saini makubaliano ambapo wanahisa walikubali marekebisho ya kampuni hizo mbili na baada ya hapo TTCL na Celtel zikawa kampuni tofauti kabisa kisheria, kifedha na kiuendeshaji.[6]

SaskTel

hariri

Mwaka 2006, TTCL ilikabiliwa na changamoto kadhaa za fedha na uendeshaji ambazo zilitishia uhai wa muda mrefu wa kampuni. Mnamo Februari 2007, wanahisa waliipa kampuni ya Kanada, SaskTel, kandarasi ya miaka mitatu ya usimamizi ili kuongoza mabadiliko ya teknolojia, kifedha, kiutendaji na kiutamaduni ya TTCL. Mkataba huo ulihitaji timu mpya ya uongozi wa juu kuboresha nafasi ya ushindani ya muda mrefu ya TTCL na kukuza idadi ya wateja wake na vyanzo vya mapato. SaskTel International ilichukua uongozi wa TTCL Julai 2007. Hata hivyo, kutoelewana kati ya SaskTel na wanahisa walio wengi juu ya mpango wa muda mrefu wa ufadhili wa mtaji wa TTCL, uliojadiliwa na SaskTel kusaidia mpango wa ukuaji, ulisababisha tarehe 12 Julai 2009 SaskTel kuwasilisha notisi ya siku 45 ya kusitisha kandarasi na kumaliza mkataba wa usimamizi. Wakati Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL iliidhinisha mpango wa ufadhili, wanahisa wengi walikataa kuunga mkono mpango huo na kusababisha timu ya wasimamizi wakuu wa SaskTel kuondoka rasmi kwenye shirika hilo mnamo Septemba 2009.[7]

Uhamisho wa hisa

hariri

Mnamo Septemba 2013 Kampuni Kuu ya Celtel MTC Group ilinunuliwa na Zain International BV ya Kuwait.[8] Pamoja na chapa ya celtel, Zain pia ilipata hisa 35% katika TTCL. Kuanzia makubaliano ya nwaka wa 2005 Celtel na TTCL zilitambuliwa kama vyombo tofauti vya kisheria, kwa hivyo, Zain haikuwa na udhibiti wa moja kwa moja juu ya shughuli za kampuni. Vile vile tarehe 8 Juni 2010, Bharti Airtel ilifikia makubaliano ya ununuzi wa huduma za simu katika nchi 15 za Afrika kutoka Zain na kurithi hisa za TTCL.[9]

Kutaifisha

hariri

Mnamo Februari 2016, Bharti Airtel mmiliki wa asilimia 35 ya hisa katika kampuni ya simu ya serikali alikubali kuuza hisa zake kwa serikali kwa 14bn/-.[10] Mzozo kati ya kampuni hiyo na serikali ulidumu kwa miaka mitatu huku kampuni hiyo ikidai pesa zaidi za fidia.[11][12] Hata hivyo, mauzo yalihitimishwa tarehe 23 Juni 2016 na kampuni ikarejea kuwa mali ya serikali.[13]

Maswala ya ushirika

hariri

Umiliki

hariri

Hivi sasa kampuni hiyo inamilikiwa kwa asilimia zote na Serikali. Mwaka 2001 serikali ya Tanzania iliuza hisa 35% za kampuni na mwaka 2016 ili kulinda kampuni hiyo, ilinunua tena hisa hizo ili kurejesha umiliki wa asilimia 100. Washirika wa mwisho wa kampuni hiyo walikuwa Bharti Airtel ya India[14][15]

Mwenendo wa biashara

hariri

Hadi kufikia Machi 2016 TTCL ilikuwa na wateja wachache kuliko watoa huduma wengine sita wa simu za mkononi nchini. TTCL ina jumla ya wateja 305,000 ambapo asilimia 45 ni watumiaji wa simu za mezani. Katika soko la simu za mezani, TTCL inakaribia kuwa na ukiritimba na inashughulikia zaidi ya asilimia 99 ya wateja.[16]

2010 2011 2012 2013 2014 2015 2016
Mauzo (TSh. billion/=) 80 93 96 104 119
Mauzo (US$ million)* 57.5 55.1 57.7 49.5 54.5
Faida/hasara (TSh. billion/=) -28 -16
Wateja 252,813 226,153 227,424 209,111 288,136 303,186
Vidokezo/vyanzo [17] [18] [19] [20] [21][22] [23][22] [22]

Makao Makuu

hariri

Kampuni hii ina makao yake makuu na kituo cha huduma kwa wateja katika Jengo la Extelecom lililopo Barabara ya Samora, mashariki mwa Kisutu, kusini mashariki mwa Dar es Salaam.

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) pia linasimamia na kuendesha ofisi na idara za uhandisi katika mikoa na miji mikuu yote nchini.

Angalia pia

hariri
  1. Vodacom Tanzania
  2. Airtel Tanzania
  3. MIC Tanzania Limited (tiGO)
  4. Vodacom
  5. Teknolojia ya 3G
  6. Celtel International
  7. Eastern Africa Submarine Cable System

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 "Govt Reclaims 100 Percent Shares in TTCL Ownership". Retrieved on 7 September 2016. 
  2. [1] Tanzania's leading operator TTCL, enters the next generation with an Ericsson 'Learning Solution
  3. Smith, Allan B. (1971), History of the east African posts and telecommunications administration 1837 to 1967 (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2022-08-19
  4. "The Tanzania Posts and Telecommunications corporation Act, 1977" (PDF). Government of Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-09-16. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Archived copy" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 19 Mei 2011. Iliwekwa mnamo 28 Januari 2008.{{cite web}}: CS1 maint: archived copy as title (link) The Regulatory Design Problem Revisited: Tanzania’s Pioneering Position in Africa
  6. [2] TTCL and Celtel now separate companies 22 August 2005
  7. TGC, . (6 Julai 2009). "SaskTel Pulls Out of TTCL Deal". Telegeography.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-23. Iliwekwa mnamo 28 Mei 2015. {{cite web}}: |first= has numeric name (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "Zain – about-us – milestones". Zain Group. Iliwekwa mnamo 6 Agosti 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Tripathy, Devidutta; Goma, Eman (8 Juni 2010). "Bharti closes $9 billion Zain Africa deal". Reuters. Reuters. Iliwekwa mnamo 7 Septemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Tanzania's leading provider of prepaid, postpaid mobile, Internet services & Mobile Money". Airtel. Iliwekwa mnamo 2022-08-19.
  11. "UWEKEZAJI: Serikali, Airtel wavutana hisa za TTCL". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2021-03-11. Iliwekwa mnamo 2022-08-19.
  12. "Tanzania: Govt Reclaims 100 Percent Shares in TTCL Ownership". Iliwekwa mnamo 7 Septemba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. Reporter, DAILY NEWS. "State in full ownership of TTCL". dailynews.co.tz. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-26. Iliwekwa mnamo 7 Septemba 2016. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. "Tanzanian government takes back 35% of TTCL from Airtel to regain full ownership" (kwa American English). 27 Mei 2015. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. "Airtel Waijibu Serikali Kuhusu Sakata la Ubinafsishaji wa TTCL - Global Publishers". globalpublishers.co.tz. Iliwekwa mnamo 2022-08-17.
  16. "March 2016 communication statistics" (PDF). tcra.co.tz. Machi 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-11-19. Iliwekwa mnamo 2022-08-17.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  17. Majaliwa. "Govt Reclaims 100 Percent Shares in TTCL Ownership". AllAfrica. Iliwekwa mnamo 2022-08-17.
  18. "TCRA Statistics 2011" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2019-04-07. Iliwekwa mnamo 2022-08-17.
  19. "TCRA Statistics 2012" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2019-04-07. Iliwekwa mnamo 2022-08-17.
  20. "TCRA Statistics 2013" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2019-04-07. Iliwekwa mnamo 2022-08-17.
  21. "TCRA Statistics 2014" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2019-04-07. Iliwekwa mnamo 2022-08-17.
  22. 22.0 22.1 22.2 "We're in good shape to issue dividend to govt, says TTCL", The Citizen, 2018-03-07. (en) 
  23. "TCRA statistics 2015" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-11-18. Iliwekwa mnamo 2022-08-17.