Mfumo katika soka

(Elekezwa kutoka Mfumo "katika soka")

Mfumo katika soka ni mpangilio wa wachezaji wa timu kwenye uwanja. Mifumo mbalimbali inaofautiana katika idadi ya wachezaji waliopangwa kama washambuliaji, viungo na mabeki. Mfumo wa aina hii unaleta tofauti kama timu inalenga kukaza zaidi mashambulio au utetezi katika mechi.

Programu ya mchezo baina ya Blackburn Rovers dhidi ya Sheffield Wednesday ya mwaka 1887. Wachezaji wamejipanga katika mfumo wa 2–3–5.

Soka ni mchezo wa haraka na wa mabadiliko mengi na nafasi ya mchezaji awapo uwanjani haimaanishi ana majukumu fulani pekee (acha golikipa). Hata hivyo uwepo wa mchezaji katika nafasi fulani huelezea kama ana majukumu ya kukaba zaidi au kushambulia zaidi, na kama wanacheza upande mmoja wa uwanja au katikati.

Mfumo mara nyingi huelezewa kutumia namba tatu au nne, namba hizi zinaelezea idadi ya wachezaji katika nafasi fulani. Mfano, mfumo maarufu wa "4–5–1" unakuwa na mabeki wanne, viungo watano na mshambuliaji mmoja. Mifumo tofauti hutumika kulingana na mategemeo ya timu katika mchezo fulani, kama wanategemea kushambulia zaidi au kukaba zaidi, na timu huweza kubadili mifumo kati ya mechi tofauti au wakati wa mechi moja.

Chaguo la mfumo hufanywa na kocha. Uwezo wa wachezaji huhitajika mara zote katika kutekeleza majukumu yanayotokana na mfumo unaotumika. Chaguzi la mfumo hufanywa kuzingatia wachezaji waliopo kwa wakati fulani. Baadhi ya mifumo iliundwa ili kukazia na kuongeza nguvu kwa baadhi ya nafasi na wachezaji.

Wakati soka lilipoanza, mifumo iliyotumika ilitumia washambuliaji wengi, tofauti na sasa ambapo walinzi au beki ni wengi kuliko washambuliaji.

Jamii ya Mifumo

hariri

Mifumo huelezewa kwa namna wachezaji wanavyojipanga uwanjani bila kumuhesabu golikipa, kuhesabu wachezaji katika mfumo hufanywa kwa kufuata marefu ya uwanja na sio mapana, kundi la kwanza ni la beki au wachezaji wenye uwezo wa juu wa kukaba. Mfano katika namba 4–4–2 hii humaanisha kuna mabeki wane, viungo wanne na washambuliaji wawili.

Kwa kawaida, wachezaji wanaochea katika nafasi moja (mfano viungo wane katika 4-4-2) hucheza katika mstari ulionyooka huku wachezaji wawili wa pembeni kulia na kushoto wakicheza juu kidogo. Katika soka la kisasa, huwa kuna mabadiliko madogo hii imesababisha baadhi ya wachambuzi kuwagawa wachezaji hawa katika makundi mawili tofauti, inayoleta mifumo yenye namba nne au tano. Fano uliozoeleka ni wa 4–2–1–3, Katika huu mfumo, viungo wamegawanywa katika makundi mawili, viungo wakabaji wawili na kiungo mshambuliaji mmoja, hata na hivyo mfumo huu unajulikana kama aina mojawapo ya mfumo wa 4–3–3. Mfano mzuri wa mfumo wenye namba tano ni 4–1–2–1–2, hapa viungo wamegawanywa katika makundi amtatu, kiungo mkabaji mmoja, viungo wa kati wawili na kiungo mshambuliaji mmoja; mfumo huu unajumuishwa katika mfumo wa 4–4–2 (hasahasa 4–4–2 umbo la almasi).

Matumizi ya namba katika mifumo haikuwepo hapo kabla, ilianza kutumika katika miaka ya 1950 mfumo wa 4-4-2 ulipoanzishwa.

Chaguzi na matumizi ya mifumo

hariri

Kwa kawaida chaguzi la mfumo wa kutumika huendana na aina ya wachezaji waliopo katika timu.

  • Mifumo miembamba. Kwa timu zenye matumizi makubwa ya viungo wa kati au zinazoshambulia zaidi kupitia katikati wanaweza kuchagua kutumia mifumo ya aina hii, mifumo kama 4–1–2–1–2 au 4–3–2–1 huruhusu timu kuwa na viungo wane hadi watato. Hata na hivyo mifumo ya aina hii hutegemea kwa kiasi kikubwa beki wa pembeni kupanda kucheza kama winga wakati wakiwa wanashambulia.
  • Mifumo mipana. Kwa timu zenye matumizi makubwa ya washambuliaji na winga wanaweza kuchagua matumizi ya mifumo hii, mfumo kama 4–2–3–1, 3–5–2 na 4–3–3, inawasukuma washambuliaji na winga juu kabisa ya uwanja. Mifumo mipana hufanya timu inayoshambulia kutanua uwanja hivyo kulazimisha beki wa timu pinzani kucheza sehemu kubwa ya uwanja.

Timu zinaweza kubadili mifumo wakati wowote wa mchezo ili kusaidia kusudi la wakati huo:

  • Kubadili kwenda mfumo wa kushambulia. Kama timu itakua inahitaji matokeo ya ushindi, mara nyingi huongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji kwa kutoa mchezaji kwenye nafasi mojawapo za nyuma na kumuweka kama mshambuliaji. Mfano timu inaweza kubadili kutoka 4–5–1 kwenda 4–4–2, 3–5–2 kwenda 3–4–3, au hata 5–3–2 kwenda 4–3–3.
  • Kubadili kwenda mfumo wa kuzuia. Timu inapokua inaongoza katika mchezo na ina mpango wa kuzuia na kubaki na magoli hayo, kocha anaweza kuamua kugeuza mfumo kuwa wa ukabaji zaidi, hii inaweza kua kwa kupunguza idadi ya washambuliaji na kuongeza beki au viungo wakabaji. Mfano mzuri ni mabadiliko kutoka 4–4–2 kwenda 5–3–2, 3–5–2 kwenda 4–5–1, au hata 4–4–2 kwenda 5–4–1.

Mifumo ya awali

hariri

Katika michezo ya karne ya 19, soka la kuzuia halikuchezwa kabisa, vikosi vilipangwa kuwa vya kushambulia zaidi.

Katika mchezo wa Uingera dhidi ya Uskoti tarehe 30 Novemba 1872, Uingereza ilitumia washambuliaji saba had inane katika mfumo wa 1–1–8 au 1–2–7 huku Uskoti ikiumia mfumo wa 2–2–6. Kwa uingereza, mchezaji mmoja alibaki nyuma na alipokea mipira iliyopigwa bila malengo na wachezaji wawili au mmoja walicheza katikati ili kupokea na kupiga mipira mbele walipo wachezaji wengine. Kwa wakati huo, aina ya uchezaji wa timu ya uingereza ulitegemea zaidi uwezo binafsi na wachezaji wao walijulikana sana kwa uwezo wao wa kukokota mipira. Wachezaji walikokota mipira kuelekea mbele kwa kadri wawezavyo na endapo tu waliposhindwa kuendelea mbele ndipo walipopiga mbele ili mchezaji mwingine ajaribu kuikokota. Uskoti waliwashangaza uingereza kwa kupiga pasi zenye malengo baina yao. Wachezaji wa Uskoti walipangwa katika pea, na kila mchezaji alitakiwa kutoa pasi kwa mchezaji aliyepangiwa katika pea. Cha ajabu ni kwamba, ijapokua mchezo ulikua wa kushambuliana zaidi uliisha nsuluhu ya bila kufungana.

Mifumo ya zamani

hariri

2–3–5 (Piramidi)

hariri
 
Mfumo wa piramidi

Mfumo wa kwanza wenye mafanikio na wa muda mrefu katika soka ulinakiliwa mwaka 1880.[1], hata na hivyo, katicha chapisho la mwaka 1960 na Caxton, yafuatayo yalinukuliwa ukarasa wa 432 Vol II: "Wrexham ... Mshindi wa kwanza wa kombe la whales mwaka 1877 ... kwa mara ya kwanza nchini Wales na labda uingereza, timu imecheza ikiwa na nusu beki watatu na washambuliaji watano..."

Mfumo wa 2–3–5 mwanzoni ulijulikana kama "Piramidi". Miaka ya 1890, ulikua ndio mfumo maarufu nchini uingereza na ulisambaa kwa kasi dunia nzima. Kulikua na mabadiliko machache sana na ulitumika na timu nyingi kubwa katika miaka ya 1930.

Kwa mara ya kwanza, usawa kati ya washambuliaji na mabeki ulifikiwa. Wakati wa kukaba, beki wa pembeni hukaba kwa nafasi washambuliaji wa timu pinzani, wakati huo viungo wakishuka kuziba nafasi inayoacha na mabeki hao.

Mfumo huu ulitimika na timu ya taifa ya Uruguay kushinda mashindano ya olimpiki ya mwaka 1924 na 1928 na hata mashindano ya fainali za kombe la dunia za mwaka 1930.

Ni mfumo huu ndio ulilea matumizi ya namba katika jezi.[2]

Shule ya Danubi

hariri

Maendeleo ya mfumo wa 2–3–5 ulizaa mfumo mpya kwa jina la ‘’The Danubian School’’, katika mfumo huu, washambuliaji hucheza katika nafasi za chini kidogo. Ilitumika kwa kiasi kikubwa na timu ya taifa ya Austrian, Czech na Hungari miaka ya 1920, timu iliyofanikiwa zaidi ikiwa ile ya Austrian miaka ya 1930. Mfumo ulitegemea zaidi mchezo wa pasi fu[pi fupi na uwezo binafsi wa wachezaji. Mfumo huu ulihamasishwa zaidi na mapendekezo ya bwana Hugo Meisl na Jimmy Hogan, kocha wa kiingereza waliotembelea Austria kwa mara ya kwanza.

Metodo (2–3–2–3)

hariri
 
mfumo wa Metodo

Mfumo wa metodo ulianzishwa na Vittorio Pozzo, kocha wa timu ya taifa ya Italia miaka ya 1930.[3] Huu ulikua kama muendelezo wa mfumo wa ‘’Danubian School’’. Ulikua na asili ya mfumo wa 2–3–5; ili wachezaji wa nyumba kupata nguvu zaidi wakati wa kukaba, bwana Pozzo aligundua kuwa kwa kuvuta washgambuliaji wawili nyuma kati ya watano waliokuwa hapo awali angefanikiwa kupata mahitaji aliyoyataka, kwa kufanya hivyo ndipo mfumo wa 2–3–2–3 ulipopatikana. Mfumo huu ulitengeneza safu imara ya ulinzi zaidi ya mifumo mingine yote iliyokua ikitumika kwa wakati huo pamoja na mashambulizi ya kushtukiza yenye manufaa zaidi. Timu ya taifa ya Italia ilifanikiwa kushinda mataji ya fainali za kombe la dunia mara mbili mfululizo, mwaka 1934 na mwaka 1938. Kumekua na madai kwamba klabu ya F.V Barcelona na Bayern Munich vilitumia mfumo huu chini ya kocha Pep guardiola.[4]

 
mfumo wa WM

Mfumo wa WM, wenye jina kutokama na maumbo yanayotengenezwa kutokana na nafasi za wachezaji uwanjani uliundwa katikati ya miaka ya 1920 na bwana Herbert Chapman alipokua Arsenal, hii ilikua mbinu ya kuendana na mabadiliko katika sheria ya ‘’off side’’ ya mwaka 1925. Mabadiliko ya sheria yalipelekea kupunguzwa idadi ya wachezaji pinzani katika eneo la msari wa safu ya ushambuliaji na ule wa goli kutoka watatu mpaka wawili. Hatua hii ilipelekea kuanzishwa nafasi ya beki wa kati, alipewa majukumu ya kumzuia mshambuliaji wa kati asiweze kufunga. Matumizi ya mfumo huu yalijulikana zaidi mwishoni mwa miaka ya 1930 asilimia kubwa ya vilabu vya kiingereza zilitumia mfumo wa WM. Mara kwa mara, mfumo wa WM umekua ukielezewa kama mfumo wa 3–2–5 au 3–4–3, au kwa usahihi zaidi 3–2–2–3 kuelezea herufi zinazowakilisha mfumo huu. Nafasi inayoonekana katikati ya mfumo huu baina ya winga wawili na washambuliaji wawili wa ndani viliweza kuwana nafasui nzuri klabu ya Arsenal kufanya kwa ufasaha mashambulizi ya kushtukiza. Vilabu vingi vya uingereza vilijaribu kutumia mfumo wa WM lakini havikupata mafanikio kama aliyoyapata bwana Chapman. Hii pia ilisababishwa na kukosekana wachezai wenye kaliba ya Alex James katika soka la uingereza. Alikua miongoni mwa viungo wachezeshaji wa mwanzo kabisa katika historia ya soka na mtu muhimu katika kikosi cha Arsenal kipindi Chapman akiwa kocha. Mnamo mwaka 2016, Patrick Vieira aliyeichezea Arsenal hapo kabla, kwa mara ya kwanza alipeleka mfumo huu nchini Marekani katika klabu ya New York City FC.[5]

Mfumo wa WW ni muendelezo wa mfumo wa hapo nyuma wa WM, ulianzishwa na kocha wa raia wa Hungary bwana Márton Bukovi aliyegeuza mfumo wa 3–2–5 WM kuwa 2–3–2–3 kwa kugeuza tu herufi M juu chini.[6] Kukosekana kwa mshambuliaji wa kati mwenye nguvu na uwezo ulimlazimu kumrudisha mchezaji mmoja chini kucheza kama kiungo mchezeshaji huku viungo wa kati wakiwa na majumkumu ya kukaba zaidi. Mabadiliko haya yalileta mfumo wa 2–3–1–4, ambao ulibadilika na kuwa 2–3–2–3 wakati wote timu ilipokua inakaba au haina umiliki wa mpira.

3–3–4

hariri

Mfumo wa 3–3–4 ulifanana sana na WW, tofauti pekee ikiwa ni mfumo huu kuwa na washambuliaji wa ndani waliochezeshwa zaidi sehemu ya katikati wakiambatana na winga nusu wawili. Mfumo huu ulipata umaarufu zaidi mwishoni wa miaka ya 1950 na mwanzoni mwa miaka ya 1960. Waliopata mafanikio zaidi kwa kutumia mfumo huu ni klabu ya Tottenham Hotspur mwaka 1961, katika safu ya viungo waliwatumia zaidi Danny Blanchflower, John White na Dave Mackay. Porto walishinda taji la ligi ya Ureno msimu wa 2005-06 maarufu kwa jina la Primeira Liga kwa kutumia mfumo huu chini yya kocha wao bwana Co Adriaanse.

4–2–4

hariri
 
mfumo wa 4–2–4

Mfumo wa 4–2–4 unajaribu kujumuisha lengo la kushambulia na kukaba kwa nguvu wakati wote wa mchezo, ulitokana na ugumu wa kunyumbulika kwa mfumo wa WM wakati wa mchezo. Mfumo huu unaweza elezewa pia kama muendelezo mwa mfumo wa WW. Mfumo huu ndio wa kwanza kuelezewa kwa kutumia namba.

Wakati uanzishwaji wa mfumo wa 4–2–4 unasemekana ni wa bwana Márton Bukovi, sifa za kuuendeleza hupewa watu wawili bwana Flávio Costa, Kocha wa timu ya taifa ya Brazili mwanzoni mwa miaka ya 1950, na bwana Béla Guttman. Mbinu hizi zilionekana kukua kwa njia tofauti kati ya nchi mbili, wabrazili wakijadili lakini wahungary wakifanyia kazi mawazo hayo.[6][7][8] Hata na hivyo, mfumo huu ulikuzwa na kutumika kwa ufasaha zaidi nchini Brazili katika mwishoni mwamiaka ya 1950.

Katika gareti moja maarufu nchini Brazili kwa jina la O Cruzeiro, bwana Costa alichapisha mawazo yake akiyapa jina la "diagonal system", kwa kutmia schematiki kama zilizotumika katika Makala hii, alitumia namba kuelezea mfumo kwa mara ya kwanza katika historia ya soka.[7]

4–2–4 ilitumika kwa ufasaha zaidi katika nchi ya Brazilngazi ya klabu, klabu hizi zikiwa ni Palmeiras na Santos, na ulitumiwa na timu ya taifa ya Brazil mwaka 1958 na kufanikiwa kushinda taji la kombe la dunia, zote zikiwatumia wachezaji maarufu Pelé, na Mário Zagallo. Baada ya mafanikio ya Brazili, mfumo huu ulisambaa kwa haraka sana duniani kwote. Chini ya kocha wao Jock Stein, klabu ya Celtic kwa kutumia mfumo huu ilishinda Kombe la Ulaya msimu wa 1966–67 na walifanikiwa kufika fainali msimu wa 1969–70.

Mifumo pungufu

hariri

Mchezaji akitolewa nje ya uwanja kwa sababu ya kitendo kisicho cha kiungwana wakati wa mchezo, mfano kwa kuonyeshwa kadi nyekundu au kuumia na kutokuwepo uwezekano wa kubadilisha mchezaji kutokana na sheria, timu mara nyingi hurudi nyuma katika mfumo wa kukaba zauidi kuwa 4–4–1 au 5–3–1. Katika hali isiyo ya kawaida timu inapotafuta ushindi ndipo itashambulia zaidi hata ikiwa na wachezaji pungufu uwanjani wanaweza kutumia mfumo wa 4–3–2 au hata 4–2–3.


Marejeo

hariri
  1. Murphy, Brenden (2007). From Sheffield with Love. SportsBooks Limited. uk. 83. ISBN 978-1-899807-56-7.
  2. "England's Uniforms — Shirt Numbers and Names". Englandfootballonline.com. Iliwekwa mnamo 28 Juni 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Ingle, Sean. "Knowledge Unlimited: What a refreshing tactic (November 15, 2000)", The Guardian, 15 November 2000. Retrieved on 10 July 2006. 
  4. Wilson, Jonathan. "The Question: Are Barcelona reinventing the W-W formation?", The Guardian, 26 October 2010. 
  5. Araos, Christian. "NYCFC comfortable in unconventional formation". Empire of Soccer. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-18. Iliwekwa mnamo 12 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 "Gusztáv Sebes (biography)". FIFA. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-12-08. Iliwekwa mnamo 10 Julai 2006.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 7.0 7.1 Lutz, Walter (11 Septemba 2000). "The 4–2–4 system takes Brazil to two World Cup victories". FIFA. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Januari 2006. Iliwekwa mnamo 10 Julai 2006. Archived 9 Januari 2006 at the Wayback Machine.
  8. "Sebes' gift to football". UEFA. 21 Novemba 2003. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Novemba 2003. Iliwekwa mnamo 10 Julai 2006.