Michelle Finn

ukarasa wa maana wa Wikimedia

Michelle Finn (alizaliwa Desemba 16, 1989) ni mkimbiaji wa Ireland anayeshindana kwenye mita 3000 za kuruka vikwazo. Aliiwakilisha Ireland kwenye mbio ya mita 3000 za kuruka vikwazo kwenye Olimpiki ya majira ya joto 2016 huko Rio; alimaliza wa kumi na moja kwenye joto lake.huko nyuma aliiwakilisha Ireland katika michuano ya Dunia 2015.

Finn mnamo 2019
Finn mnamo 2019

Wasifu

hariri

Finn amekualia  Castlemagner.[1] Alizaliwa Desemba 16 1989 na Mary na Toddy Finn.[2]

Finn alikuwa mwanafunzi wa mwaka wanne wa riadha kwa chuo kikuu Western Kentucky[3] akisomea mawasiliano.[4] Alipokea shahada ya pili ya lishe.Pia alikaa miaka miwili kwenye chuo kikuu Limerick.[2]

Alishika nafasi ya pili kwenye michuano nje ya nchi ya GloHealth iliyomfanya afuzu kushindana kwa ajili ya Ireland kwenye michuano ya nje ya nchi ya Ulaya 2014 iliyofanyika Bulgaria.Timu ilishinda medali ya shaba na alikuwa wa 23 kwenye tukio.

Alifuzu kwa michuoano ya dunia 2015 na olimpiki ya majira ya joto 2016 baada ya kukimbia kwa 9:43.34 kwenye 2015 Letterkenny AC International.[5] Finn alimaliza mita 3000 za kuruka vikwazo ndani ya 9:55.27 akiwa wa tisa kwa joto lake kwenye michuano ya dunia 2015. Hakuendelea mbele kufikia fainali.[6]

Finn alikimba mita 3000 za kuruka viunzi kwenye olimpiki ya majira ya joto 2016 huko Rio.Aliwapita washindani watatu wakati wa kunyoosha mara ya mwisho akamaliza wa 11 kwa muda wa 9:49.45[7] [8]alikuwa na wakati wa 39 wa haraka kwenye joto lake  na hakwenda mbele kwenye fainali.[9]

Februari 2018, Finn alivunjika mguu wake na kwa sababu hiyo ilibidi abadilishe  ratiba yake ya mafunzo ili aweze kwenda sawa na hilo.[10] Ili kufunzu kwa michuano ya Ulaya, Finn alitakiwa kukimbia 9:55 kwenye matukio mawili ya kufuzu. Julai 18 alimaliza riadha huko france kwa 9:51.43, akabakisha mara moja nyingine kufuzu kwa michuano ya Ulaya. Kwenye kuruka maji kwa mara ya kwanza kwenye mbio Julai 25,Finn alianguka vibaya na kuteguka  kisigino.Alifikiria kuacha mbio hizo lakini aliendelea na siku nne baadae alifuzu na kwa uthibitisho wa daktari wake, alikimbia kwenye michuano ya riadha Ireland,akamaliza kwa 9:46.19.[11] Kwenye michuano ya Ulaya 2018 alimaliza wa 16 kwenye joto lake kwa muda wa 10:10.93.[12]

Alifuzu kwa michuano ya dunia 2019 huko Qatar. Alimaliza wa tisa  kwenye joto lake  kwa muda wa 9:47.44, akasema kuwa muda wake uliathiriwa na kuamua vibaya kwenye kikwazo cha kwanza.[13] Juali 2019, Finn aliweka PB ya 9:41.23 wakati wa mbio huko Finland.[14] Finn alishinda  Sydney Track Classic na akaboresha ubora wake  kwa muda wa  9:38.04.[15]Finn aliyejiunga na klabu ya riadha ya Melbourne januari 2020 anajifunza kwa ajili ya olimpiki ya majira ya joto itakayofanyika Tokyo.[16]

Marejeo

hariri
  1. "Blake, John Clifford, (12 July 1901–13 March 1993)", Who Was Who, Oxford University Press, 2007-12-01, iliwekwa mnamo 2021-10-06
  2. 2.0 2.1 ""Jete" wins cross country". doi:10.31096/wua044-vms_406a_box_3. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)
  3. "Trafford, Ian Colton, (8 July 1928–24 March 2011), Publisher, The Times Supplements, 1981–88", Who Was Who, Oxford University Press, 2007-12-01, iliwekwa mnamo 2021-10-06
  4. "Contemporary Japan, Volume 10, Issue 03 - 1941 March". Manchuria Daily News Online. Iliwekwa mnamo 2021-10-06.
  5. "Arnott, Sir John, (1817–28 March 1898), proprietor of Irish Times", Who Was Who, Oxford University Press, 2007-12-01, iliwekwa mnamo 2021-10-06
  6. "Arnott, Sir John, (1817–28 March 1898), proprietor of Irish Times", Who Was Who, Oxford University Press, 2007-12-01, iliwekwa mnamo 2021-10-06
  7. "Went, David, (born 25 March 1947), Chairman, Irish Times Ltd, 2007–13", Who's Who, Oxford University Press, 2007-12-01, iliwekwa mnamo 2021-10-06
  8. Ogueta-Alday, Ana; Muñoz Molleda, Fernando; García-López, Juan (2015-03-06). "Análisis biomecánico de la competición de 3000 m obstáculos (Biomechanical analysis of the 3000 m steeplechase competition)". Retos (26): 157–162. doi:10.47197/retos.v0i26.34424. ISSN 1988-2041.
  9. Ogueta-Alday, Ana; Muñoz Molleda, Fernando; García-López, Juan (2015-03-06). "Análisis biomecánico de la competición de 3000 m obstáculos (Biomechanical analysis of the 3000 m steeplechase competition)". Retos (26): 157–162. doi:10.47197/retos.v0i26.34424. ISSN 1988-2041.
  10. "Mccolgan-Nuttall, Elizabeth, (born 24 May 1964), athletic coach; Director: Athletic Zones; Doha Athletic Club; RunDohaRun", Who's Who, Oxford University Press, 2007-12-01, iliwekwa mnamo 2021-10-06
  11. "[Illustrations]", Notre Dame vs. The Klan, University of Notre Dame Press, 2018-08-15, iliwekwa mnamo 2021-10-06
  12. "Spring Meeting Minutes - FINAL, Board of Educational Affairs (BEA), March 23 - March 25, 2018". PsycEXTRA Dataset. 2018. Iliwekwa mnamo 2021-10-06.
  13. "Arnott, Sir John, (1817–28 March 1898), proprietor of Irish Times", Who Was Who, Oxford University Press, 2007-12-01, iliwekwa mnamo 2021-10-06
  14. "The BBC", Learie Constantine and Race Relations in Britain and the Empire, Bloomsbury Academic, 2019, iliwekwa mnamo 2021-10-06
  15. "Arnott, Sir John, (1817–28 March 1898), proprietor of Irish Times", Who Was Who, Oxford University Press, 2007-12-01, iliwekwa mnamo 2021-10-06
  16. O'Riordan, Conal (1912). "His Majesty's Pleasure". The Irish Review (Dublin). 2 (20): 431. doi:10.2307/30062871. ISSN 2009-0978.