Popo-wadudu
Popo-wadudu | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Popo pua-njumufarasi mdogo
(Rhinolophus hipposideros) | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Familia 14:
|
Popo-wadudu ni aina za popo wanaowinda wadudu hasa. Kibiolojia ni mamalia wa nusuoda Yangochiroptera katika oda Chiroptera wanaofanana na panya wenye mabawa. Kwa kawaida spishi hizi ni ndogo kuliko zile za nusuoda Yinpterochiroptera (popo-matunda) lakini kuna spishi zilizo kubwa kulika spishi fulani za popo-matunda. Spishi ndogo kabisa ni popo nyukibambi aliye na urefu wa mm 29-33 na uzito wa g 2. Kwa hivyo popo huyu ni spishi ndogo kabisa ya mamalia pia. Kirukanjia wa Etruski anaweza kuwa na uzito mdogo zaidi (g 1.2-2.7) lakini ni mrefu zaidi (mm 36-53). Popo-wadudu hula wadudu hasa lakini spishi nyingine hula samaki, ndege na wanyama wadogo na hata damu. Hutumia miwangwi ya sauti yao ili kuyakamata mawindo yao. Spishi kadhaa hula matunda na mbochi na hizi hazitumii miwangwi.
Oda: Chiroptera
- Nusuoda Yangochiroptera
- Familia Cistugidae (Popo mabawa-tezi)
- Familia Emballonuridae (Popo mkia-uo)
- Familia Furipteridae (Popo bila gumba)
- Familia Miniopteridae (Popo mabawa-marefu)
- Familia Molossidae (Popo mkia-huru)
- Familia Mormoopidae (Popo uso-pepo)
- Familia Mystacinidae (Popo mkia-mfupi wa Nyuzilande)
- Familia Myzopodidae (Popo miguu-minaso)
- Familia Natalidae (Popo masikio-mpare)
- Familia Noctilionidae (Popo wavuvi)
- Familia Nycteridae (Popo uso-kibonde)
- Familia Phyllostomidae (Popo pua-jani)
- Familia Thyropteridae (Popo mabawa-minaso)
- Familia Vespertilionidae (Popo-jioni)
Picha
hariri-
Popo mkia-uo wa Pasifiki
-
Popo uso-kibonde wa Misri
-
Popo-jioni rangi-mbili
-
Popo mkia-huru wa Mexiko
-
Popo masikia-mpare wa Mexiko
-
Popo mvuvi mkubwa
-
Popo uso-pepo
-
Popo pua-mshale mweupe
Marejeo
hariri- ↑ James M. Hutcheon and John A.W. Kirsch (2006). "A moveable face: deconstructing the Microchiroptera and a new classification of extant bats". Acta Chiropterologica. 8: 1–10. doi:10.3161/1733-5329(2006)8[1:AMFDTM]2.0.CO;2.