Miikka Mwamba
Miikka Aleksanteri Kari (amezaliwa tar. 16 Oktoba 1971, mjini Helsinki, Ufini) ni mtayarishaji wa muziki na mhandisi wa sauti toka nchini Ufini-Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kitayarishaji kama Miikka Mwamba. Miikka Mwamba ni mtayarishaji mashuhuri sana kwa nchi ya Tanzania, na ameweza kujibebea umaarufu mkubwa sana nchini Tanzania kunako miaka ya 2000.
Miikka Mwamba | |
---|---|
![]() Miikka Mwamba.
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Miikka Aleksanteri Kari |
Amezaliwa | 16 Oktoba 1971 |
Asili yake | Finland |
Aina ya muziki | Hip hip R&B Dansi Pop |
Kazi yake | Mtayarishaji |
Studio | Mwamba Productions FM Studio Kokwa Records |
Tovuti | Mwambaproductions.com |
Miikka aliwahi kufanya kazi na wasanii mbalimbali wa nchini Tanzania. Wasanii hao ni: Dully Sykes, Inspector Haroun, Lady Jay Dee, Mad Ice, Chegge, Mandojo na Domo Kaya, Solid Ground Family, Complex, Zahrani (maarufu kama Big Punisher wa Bongo), Only Face, Dknob na wengine wengi wa kutoka Tanzania.
Miikka Mwamba, ameshawahi kufanya kazi miaka mingi kwenye medani za muziki, filamu, michezo ya kuigiza na dansi, ni swala ambalo si mara nyingi kufanyika kwa nchi ya Ufini na Tanzania pia.
Miikka alihitimu elimu yake ya msingi na secondary katika Lohja, ambacho ni chuo cha sanaa (Torkkelin kuvataidelukio) alisomea Helsinki, na shahada ya uzamili (MA) alipata Theatre Academy of Finland, Dept. of Light and Sound Design.