Mikoa ya Uholanzi ni ngazi ya utawala kati ya serikali ya kitaifa na manisipaa au kata. Uholanzi hugawiwa kwa mikoa 12 (provincies kwa Kiholanzi).

Mikoa ya Uholanzi


Muundo na madaraka ya utawala

hariri

Kila mkoa unatekeleza wajibu zinazokabidhiwa kwake na serikali kuu. Mkoa huwa na bunge ya kimkoa inayoitwa "Provinciale Staten", halafu kamati ya utendaji ya "Gedeputeerde Staten" inayosimamiwa na "Commissaris van de Koningin" au kamishna wa malkia anayeteuliwa na serikali ya kitaifa kwa niaba ya malkia.

Hata kama kila mkoa huwa na bunge na kamati ya serikali haiwezi kuitwa "jimbo" kwa sababu madaraka yake si makubwa. Serikali ya kitaifa ina haki ya kubadilisha mikoa lakini mipaka imekaa vile tangu karne ya 19.

Mkoa unasimamia hasa kazi ya manisipaa na kata halafu shughuli za hifadhi mazingira, ustawi wa jamii na utamaduni kwa eneo lake. Katika wajibu hizi inapaswa kufuata masharti yanayotolewa na wizara za serikali kuu. Pesa yake inapokea kutoka makisio ya kitaifa lakini ina haki ya kuamua kimkoa juu ya kodi ya magari.

Mikoa 12 inaorodheshwa hapo chini pamoja na miji penye makao makuu:

Mkoa Mji mkuu
Groningen Groningen
Friesland Leeuwarden
Drenthe Assen
Overijssel Zwolle
Gelderland Arnhem
Utrecht Utrecht
Flevoland Lelystad
Noord-Holland Haarlem
Zuid-Holland Den Haag (The Hague)
Zeeland Middelburg
Noord-Brabant ’s-Hertogenbosch (Den Bosch)
Limburg Maastricht


Viungo vya Nje

hariri