Ruaha Mkuu (pia: Ruaha Mkubwa) ni mto muhimu nchini Tanzania na tawimto la Rufiji. Huitwa "Ruaha Mkuu" kwa kuutofautisha na "Ruaha Mdogo" unaoishia ndani yake, si mbali na Iringa Mjini.

Mandhari ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na mto wake tarehe 27 Julai 2003.
Mto Ruaha

Jina Ruaha kwa Kihehe linamaanisha "maji mengi".

Chanzo na mwendo wa mto

hariri

Chanzo chake ni mito mingi midogo inayotelemka milima ya nyanda za juu za kusini mwa Tanzania, hasa safu za milima ya Uporoto na ya Kipengere. Mito hii inakusanya maji yake kwenye tambarare ya Usangu na ndipo Ruaha inapoanza. Mito mikubwa zaidi inayoungana hapa na kuunda Ruaha ni pamoja na mto Mbarali, mto Kimani na mto Chimala.

Karibu na Ng’iriama mto unatoka katika Usangu na kuingia hifadhi ya kitaifa ya Ruaha. Inaendelea kupokea Ruaha Mdogo na mto Kisigo kabla ya kuingia katika ziwa la lambo la Mtera, halafu inaendelea hadi lambo la Kidatu.

Baada ya Kidatu, Ruaha Mkuu unapita tambarare ya Kilombero hadi kuishia katika mto Rufiji.

Matatizo ya ekolojia ya mto

hariri
 
Ruaha Mkuu jinsi ilivyokauka mwaka 2006 kwenye eneo la Hifadhi ya taifa ya Ruaha.

Maji ya Ruaha Mkuu ni muhimu kwa ekolojia ya beseni lake pamoja na watu wote wanaoishi huko. Lakini matumizi ya binadamu yameleta mvurugo kwa ekolojia ya mto na tangu mwaka 1993 mto umeanza kukauka wakati wa ukame. Uhaba wa maji umesababishwa na matumizi mabaya ya maji upande wa miradi mikubwa ya mpunga katika Usangu.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri

7°56′S 37°52′E / 7.933°S 37.867°E / -7.933; 37.867