Milima ya Ukinga (Njombe)

Milima ya Ukinga iko kusini magharibi mwa Tanzania kwenye ncha ya kaskazini ya Ziwa Malawi.

Ni sehemu ya kusini ya Milima ya Kipengere, safu ya milima inayoelekea kusini mashariki kutoka bonde la mto Ruaha Mkuu upande wa kaskazini hadi lile la mto Ruhuhu upande wa kusini kwa kufuata Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.

Kilele chake ni Mlima Jamimbi (mita 2,925 juu ya usawa wa bahari) unaoshuka moja kwa moja ziwani.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri