Mnanasi
Mnanasi | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mnanasi
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Mnanasi (Ananas comosus) ni mmea katika familia Bromeliaceae ya oda Poales.
Mnanasi unakuzwa hasa kwa sababu ya matunda yake, yanayoitwa mananasi, na juisi inayotokana na matunda haya.
Asili yake ni Amerika ya Kusini ingawa kwa sasa unakuzwa sehemu nyingi za dunia.
Visumbufu vya mnanasi
haririVijidudu vinavyomelea mnanasi huchangia kuleta hasara kubwa kote duniani katika uzalishaji wa mananasi[1]. Spishi zaidi ya mia moja za nematodi zimeripotiwa kuingia mizizi ya mnanasi[1] na kutatiza matumizi ya madini na maji kwa mmea na kusababisha mimea kudumaa. Aina za vijidudu hivi ambavyo huadhiri mavuno ya mananasi sana ni spishi za nematodi kama vile Meloidogyne javanica, M. incognita, Rotylenchulus reniformis na Pratylenchus brachyurus[2][1].
Helicotylenchus dihystera na Criconemella ornata (kwa Kiing. Ring nematode) pia hupatikana sana kwa mashamba ya mananasi ingawa huwa hawasababishi uharibifu wowote uonekanao[3] [4].
Huko Hawaii, upungufu wa kiasi kikubwa wa uzalishaji wa mananasi umeripotiwa kutokana na uharibifu au maambukizo ya nematodi. Katika mashamba ya mananasi ya Queensland, huko Australia, M. javanica ameripotiwa kuwa spishi aliye na uharibifu zaidi kuliko aina zote za vijidudu vinavyomelea mananasi[4].
Picha
hariri-
Nanasi
-
Nematodi wa vifundo vya mizizi akiingia mzizi wa mnyanya
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 Sipes, B.S., E.P. Caswell, J. Chen Sarah & W. Apt (2005). "Nematodes parasites of pineapple". Katika M. Luc, R.A. Sikora & J. Bridge (eds.) (mhr.). Plant-Parasitic Nematodes in Subtropical and Tropical Agriculture (tol. la 2nd Edition). ku. 709-731.
{{cite book}}
:|edition=
has extra text (help);|editor=
has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ Sipes, B.S. and D.P. Schmitt (2000). "Rotylenchulus reniformis damage threshold on pineapple". Acta Horticulturea. 529: 239–246.
- ↑ Raski, D. J. and Krusberg, L.R. (1984). "Nematode parasites of grapes and other small fruits". Katika W.R. Nickle (ed.) (mhr.). Plant and insect nematodes. New York: Mercel Dekker inc. ku. 457–506.
{{cite book}}
:|editor=
has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ 4.0 4.1 Stirling, G.R. (1993). "Nematodes". Katika Broadley, RH, Wassman, RC and Sinclair, E (eds.) (mhr.). Pineapple: Pests and Disorders. Brisbane: Queensland Department of Primary Industries. ku. 21–29.
{{cite book}}
:|editor=
has generic name (help)CS1 maint: multiple names: editors list (link)