Mtaguso

(Elekezwa kutoka Mitaguso)


Mtaguso ni mkutano wa viongozi wa Kanisa hasa maaskofu pamoja na Wakristo wengine kadhaa.

Wa kwanza ulikuwa ule wa Mitume uliofanyika Yerusalemu ili kujadili suala la waongofu wa mataifa, kama walazimishwe kutahiriwa na kufuata Torati yote au sivyo.

Waliohudhuria ni pamoja na Mtume Petro, Yakobo Mdogo, Mtume Paulo, Barnaba n.k. (Mdo 15:1-29).

Mtaguso unaweza kufanyika katika ngazi mbalimbali, kuanzia kanda, taifa hadi Mtaguso mkuu wa kimataifa.

Mitaguso saba ya kwanza ya kanisa lisilogawiwa bado inakubaliwa na Wakristo wengi kama Wakatoliki, Waorthodoksi na Waprotestanti kama mitaguso ya kiekumene.

Tangu kutokea kwa mafarakano urithi wa mitaguso umedumu hasa ndani ya Kanisa Katoliki lililoendelea kuendesha mitaguso mbalimbali.

Kati yake, mtaguso muhimu wa siku za karibuni ulikuwa Mtaguso wa pili wa Vatikano uliofanyika Roma kati ya 1962 na 1965 na kuleta hali mpya hata katika uhusiano wa Wakatoliki na Wakristo wenzao wa madhehebu tofauti, tena kati yao na ulimwengu wote.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtaguso kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.