Mtume Barnaba
Mtume Barnaba (jina la awali Yosefu wa Kupro) alikuwa Myahudi wa kabila la Lawi katika karne ya 1 BK.
Anajulikana hasa kwa jina la Barnaba (kwa Kiaramu בר נביא, bar naḇyā, yaani 'mwana wa nabii'. Lakini Luka mwinjili (kitabu cha Matendo ya Mitume 4:36) alilitafsiri kwa Kigiriki υἱός παρακλήσεως, huios paraklēseōs, yaani "mwana wa faraja" au "mwana wa himizo".
Tangu kale Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Waanglikana na Walutheri wanamheshimu kama mtakatifu tarehe 11 Juni[1].
Katika kitabu hicho cha Agano Jipya (Biblia ya Kikristo) tunapata habari kuwa aliongokea mapema Ukristo, akauza shamba lake na kuwakabidhi Mitume wa Yesu mapato yake ili wawasaidie maskini. Labda kwa sababu hiyo Mitume walimuita Barnaba (Mdo 4:36-37).
Kisha kuheshimiwa hivyo katika Kanisa la awali huko Yerusalemu, alimtambulisha na kumdhamini Mtume Paulo muda mfupi baada ya huyo kuongoka huko Damasko (Mdo 9:26Katika kitabu hicho cha Agano Jipya (Biblia ya Kikristo) tunapata habari kuwa aliongokea mapema Ukristo, akauza shamba lake na kuwakabidhi Mitume wa Yesu mapato yake ili wawasaidie maskini. Labda kwa sababu hiyo Mitume walimuita Barnaba (Mdo 4:36-37). -28).
Watu wa mataifa walipoanza kuingizwa moja kwa moja katika Ukristo mjini Antiokia, alitumwa huko kwa niaba ya Kanisa mama, akawa kiongozi mkuu wa jumuia hiyo mpya (Mdo 11:19-30; 13:1).
Baadaye Roho Mtakatifu alidai yeye na Paulo wapelekwe kufanya umisionari sehemu nyingine, wakaondoka pamoja na binamu yake, Yohane Marko, kuelekea kwanza kisiwani Kupro, halafu bara, katika maeneo ya Uturuki Kusini wa leo (Mdo 13:2-14:28).
Kazi yao ilipopata upinzani kwa sababu ya kutodai Wapagani wakiongoka washike Torati yote, walikwenda pamoja Yerusalemu (mwaka 49 hivi, kwa mtaguso wa Mitume, ambao uliamua kuhusu suala hilo (Mdo 15:1-35).
Baada ya kutengana na Paulo, Barnaba alifunga tena safari kwenda Kupro pamoja na Marko (Mdo 15:36-39) kati ya miaka 50 na 53.
Baada ya hapo hatuna tena habari ya hakika juu yake, ila Mtume Paulo alimtaja kama mfano wa mtu asiye na mke kwa ajili ya uinjilishaji (1Kor 9:16-22).
Habari nyingine
haririMapokeo yanasema aliuawa kwa ajili ya imani yake huko Salamis, Kupro, mwaka 61[2].
Wataalamu wengine wanamtaja kama mtunzi wa Waraka kwa Waebrania, na Klemens wa Aleksandria alimtaja kama mwandishi wa Waraka wa Barnaba, lakini hakuna hakika.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Attwater, Donald and Catherine Rachel John. "The Penguin Dictionary of Saints," 3rd edition, New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.
Kuhusu maandishi yake
hariri- Die Apostolischen Väter. Griechisch-deutsche Parallelausgabe. J.C.B. Mohr Tübingen 1992. ISBN 3-16-145887-7
- Der Barnabasbrief. Übersetzt und erklärt von Ferdinand R. Prostmeier. Series: Kommentar zu den Apostolischen Vätern (KAV, Vol. 8). Vandenhoeck & Ruprecht: Göttingen 1999. ISBN 3-525-51683-5
Viungo vya nje
hariri- Biography of St Barnabas Ilihifadhiwa 8 Julai 2008 kwenye Wayback Machine.
- Gospel of Barnabas
- The Ecole Glossary about Barnabas Ilihifadhiwa 30 Oktoba 2005 kwenye Wayback Machine.
- The Epistle of Barnabas
- St. Barnabas the Apostle Ilihifadhiwa 9 Novemba 2005 kwenye Wayback Machine.
- Jewish Encyclopedia: Barnabas
- Parish of St Barnabas in Tunbridge Wells, England, UK
- Barnabas Community Church, Shrewsbury, England, UK
- St Barnabas Monastery and Icon Museum, Famagusta, Cyprus
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtume Barnaba kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |