Mjoho
Mjoho | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mjoho mpweke
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Mijoho ni miti mikubwa kiasi ya jenasi Diospyros katika familia Ebenaceae. Matunda yake huitwa majoho.
Spishi kadhaa hupandwa ili kuvuna majoho, lakini spishi nyingi sana hukua misituni katika kanda za tropiki na nusutropiki. Nyingine hukatwa ili kutumia ubao wao mzuri (abunusi), nyingine hutumiwa kwa kuvuna majoho, nyingine tena hazitumiki.
Spishi nyingi hutishika na kutoweka kwa sababu zinakatwa sana au kwa sababu mazingira yao yanaharibiwa.
Spishi za Afrika
hariri- Diospyros abyssinica, Mdaa-mwitu, Mtitu au Mjoho Kaskazi
- Diospyros amaniensis, Mjoho wa Amani
- Diospyros blancoi, Mjoho Hindi
- Diospyros boutoniana, Mjoho Majani-makubwa
- Diospyros bussei, Mku au Mjoho wa Busse
- Diospyros capricornuta, Mjoho wa Pwani
- Diospyros chamaethamnus, Mjoho-mchanga
- Diospyros consanguinea, Mlalasungura
- Diospyros crassiflora, Mjoho Magharibi
- Diospyros dichrophylla, Mjoho Sumu
- Diospyros feliciana, Mjoho wa Gini
- Diospyros greenwayi, Mjoho wa Greenway
- Diospyros kaki, Mjoho Kaki
- Diospyros katendei, Mjoho wa Katende
- Diospyros leucomelas, Mjoho wa Morisi
- Diospyros lycioides, Mjoho Buluu
- Diospyros magogoana, Mjoho wa Rondo
- Diospyros melanida, Mjoho Mweupe
- Diospyros mespiliformis, Mjoho Mpweke, Mpweke, Mgiriti, Mgombe, Mngombe au Mkea-kiindi
- Diospyros nodosa, Mjoho Sepali-kubwa
- Diospyros occulta, Mjoho wa Magombera
- Diospyros pterocalyx, Mjoho Sepali-mabawa
- Diospyros revaughanii, Mjoho wa Revaughani
- Diospyros seychellarum, Mjoho wa Shelisheli
- Diospyros shimbaensis, Mjoho wa Shimba
- Diospyros squarrosa, Mhambarashi au Mpweke
- Diospyros tessellaria, Mjoho Mweusi
- Diospyros usambarensis, Mdaa
- Diospyros wajirensis, Mjoho wa Wajir
- Diospyros whyteana, Mjoho Kusi
Picha
hariri-
Majani na tunda vya mjoho hindi
-
Majani na tunda vya mjoho-mchanga
-
Majani na matunda ya mjoho sumu
-
Mti mchanga wa mjoho wa Greenway
-
Majani na matunda ya mjoho kaki
-
Mjoho wa Revaughani
-
Majani na matunda mabichi ya mhambarashi
-
Mjoho mweusi
-
Mjoho kusi