Mjusi-nyungunyungu
Mjusi-nyungunyungu | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mjusi-nyungunyungu wa Lang (Chirindia langi)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Familia 6: |
Mijusi-nyungunyungu ni wanyama watambaachi katika oda Squamata ya ngeli Reptilia. Wanyama hawa hawafikiriwi kuwa mijusi wa kweli, lakini wataalamu wengine wanafikiri kwamba wana nasaba na familia ya mijusi Lacertidae.
Kama jina lao linadokeza, mijusi-nyungunyungu wanafanana na nyungunyungu kwa sababu hawana miguu, ngozi ya takriban spishi zote ni pinki na magamba yanatungamanika katika miviringo. Hata huishi ndani ya udongo kama nyungunyungu. Kwa hivyo hawana masikio ya nje na macho yamo katika vishimo na yamefunika kwa ngozi na gamba. Wanaweza kushufu nuru kwa sababu macho bado yana kornea na lenzi.
Mijusi-nyungunyungu hula wadudu na lava wao na invertebrata wengine kama nyungunyungu.
Spishi za Afrika ya Mashariki
hariri- Agamodon anguliceps, Mjusi-nyunguyungu Kichwa-patasi (Angled worm-lizard)
- Agamodon compressus, Mjusi-nyunguyungu Bapa (Flat worm-lizard)
- Ancylocranium barkeri, Mjusi-nyunguyungu wa Lindi (Lindi sharp-snouted worm-lizard)
- Ancylocranium ionidesi, Mjusi-nyunguyungu wa Kilwa (Kilwa sharp-snouted worm-lizard)
- Ancylocranium somalicum, Mjusi-nyunguyungu Somali (Somali sharp-snouted worm-lizard)
- Chirindia ewerbecki, Mjusi-nyunguyungu wa Mbanja (Mbanja round-headed worm-lizard)
- Chirindia mpwapwaensis, Mjusi-nyunguyungu Kichwa-duara wa Mpwapwa (Mpwapwa round-headed worm-lizard)
- Chirindia rondoensis, Mjusi-nyunguyungu wa Rondo (Rondo round-headed worm-lizard)
- Chirindia swynnertoni, Mjusi-nyunguyungu wa Swynnerton (Swynnerton's round-headed worm-lizard)
- Geocalamus acutus, Mjusi-nyunguyungu wa Voi (Voi wedge-snouted worm-lizard)
- Geocalamus modestus, Mjusi-nyunguyungu Pua-kabari wa Mpwapwa (Mpwapwa wedge-snouted worm-lizard)
- Loveridgea ionidesii, Mjusi-nyunguyungu wa Liwale (Liwale round-snouted worm-lizard)
- Loveridgea phylofiniens, Mjusi-nyunguyungu wa Ujiji (Ujiji round-snouted worm-lizard)
- Pachycalamus brevis, Mjusi-nyunguyungu Mfupi (Short worm-lizard)
- Trogonophis wiegmanni, Mjusi-nyunguyungu Bao-sataranji (Checkerboard worm-lizard)