Lenzi ni kitu kilicho angavu (kama vile kioo, plastiki au hata tone la maji) ambacho kina uwezo wa kubadili taswira ya kitu kwa kupindisha miale ya nuru ambayo inapita kwenye kitu hicho. Lenzi inaweza kufanya kitu kuonekana kikubwa, kidogo, au juu-chini-chini-juu.

 Lenzi
Lenzi

Sehemu nyingine ambazo lenzi hutumika ni kwenye miwani, kamera, projekta, hadubini, darubini, vioo vya kukuza, n.k.

Kila jicho pia lina lenzi yake asili.

Huwa zinafanya kazi kwa kupindisha mwanga.

Lenzi zina maumbo matatu makuu. Kila umbo hubadilisha taswira (kuifanya iwe kubwa au ndogo). Aina tatu hizo ni:

  • Mbonyeo: sehemu ya kati ni nyembamba
  • Vungu au mbinuko: sehemu ya kati ni nene
  • Bapa

Historia

hariri

Neno "lenzi" linatokana na neno la Kiingereza Lens ambalo limetokana na Kilatini "lentil," kwa sababu lenzi za awali zilikuwa na umbo kama dengu.

Rekodi ya zamani ya maandishi ya lenzi ya Kigiriki ya Aristophanes, inatujulisha ya kwamba lenzi zilitumiwa kukusanya miale ya jua ili kufanya moto

Galileo Galilei kwa kawaida anaaminika kuwa alitumia lenzi ili kutengeneza darubini ya kwanza. Hata hivyo, yeye tu alibadilisha na kuboresha muonekano kama aliyojifunza kutoka kwa wataalamu wa Uholanzi kama vile Hans Lippershey. Huenda alikuwa ndiye wa kwanza kutumia teknolojia ili kufanya uchunguzi sahihi wa nyota.

  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.