Mkesha (Modulatricidae)
Mkesha | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mkesha kidari-madoa
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 3, spishi 3:
|
Mikesha wa familia ya Modulatricidae ni spishi tatu zilizowekwa pamoja kwa muda katika familia yao. Zamani ziliainishwa katika Timaliidae, Pycnonotidae, Turdidae na Muscicapidae lakini utafiti wa hivi karibuni imeonyesha kwamba spishi hizi zina asili ya zamani sana. Wana mnasaba na ndegesukari. Ndege hawa wanafanana na mikesha wengine bila rangi kali. Mgongo una rangi ya kahawa au kijivucheusi na chini ina rangi ya kijivu isiyoiva na madoa meusi. Hawa ni ndege wa misitu ya Afrika. Hula wadudu na pengine beri. Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika mti au kichaka au ardhini (mkesha kidari-kijivu). Jike huyataga mayai 2-4.
Spishi za Afrika
hariri- Arcanator orostruthus, Mkesha Kidari-madoa (Dapple-throat)
- Kakamega poliothorax, Mkesha Kidari-kijivu (Grey-chested Babbler)
- Modulatrix stictigula, Mkesha Koo-madoa (Spot-throat)
Picha
hariri-
Mkesha koo-madoa