Mkiwi
Mkiwi | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mikiwi ikitoa matunda
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Spishi 8 zilizo na matunda yaliwayo kwa kawaida (jumla >40):
|
Mikiwi ni mimea ya jenasi Actinidia katika familia Actinidiaceae. Mimea hii ni vichaka vyenye urefu wa hadi m 6 au mitambazi ya hadi m 30. Inazaa matunda yalikayo ambayo huitwa kiwi. Asili ya mimea hii ni Asia ya Mashariki lakini spishi kadhaa hukuzwa katika nchi nyingine, mkiwi wa kawaida (Actinidia deliciosa) hasa katika Italia na Nyuzilandi.
Spishi zinazoliwa sana
hariri- Actinidia arguta, Mkiwi Mvumilivu (Hardy kiwi au arctic kiwi)
- Actinidia chinensis, Mkiwi Njano (Golden kiwi)
- Actinidia coriacea, Mkiwi Matunda-mayai (Chinese egg gooseberry)
- Actinidia deliciosa, Mkiwi Matunda-manyoya, Mkiwi wa Kawaida au Mkiwi kwa kifupi (Fuzzy kiwi)
- Actinidia kolomikta, Mkiwi Rangirangi (Variegated kiwi vine)
- Actinidia melanandra, Mkiwi Zambarau (Red kiwi)
- Actinidia polygama, Mkiwi Fedha (Silver vine)
- Actinidia purpurea, Mkiwi Zambarau (Purple kiwi)
Picha
hariri-
Maua ya mkiwi mvumilivu
-
Matunda ya mkiwi mvumilivu
-
Maua ya mkiwi njano
-
Matunda ya mkiwi njano
-
Maua ya mkiwi matunda-manyoya
-
Matunda ya mkiwi matunda-manyoya
-
Mkiwi rangirangi
-
Matunda ya mkiwi rangirangi
-
Mkiwi fedha
-
Maua ya mkiwi fedha