Mkoa wa Gao (kwa Kibambara: Gao Dineja) ni eneo lililo kaskazini-mashariki mwa Mali. Mji mkuu ni Gao.

Ramani ya mikoa ya Gao (bado na Menaka) na Kidal
Cercles za Mkoa wa Gao

Mkoa huo unapakana upande wa kaskazini na Mkoa wa Kidal, upande wa magharibi na Mkoa wa Timbuktu. Kwa upande wa mashariki na kusini iko ncho ya Niger, halafu kuna mpaka mfupi na Burkina Faso.

Idadi ya watu hariri

Makabila katika Mkoa wa Gao ni pamoja na Wasonghai, Wabozo, Watuareg, Wabambara na Wakounta.

Wilaya hariri

Kwa madhumuni ya kiutawala, Mkoa wa Gao umegawanywa katika wilaya (cercles): [1]

Jina la Cercle Eneo (km2) Idadi ya watu

Sensa ya 1998

Idadi ya watu

Sensa ya 2009

Asongo 23,614 82,398 132,205
Bourem 43,000 80,667 115,958
Gao 31,250 143,300 239,853
Menaka 73,664 35,177 56,104

Mnamo mwaka 2016 maeneo ya Menaka yalianza kutengwa na kuwa mkoa wa pekee.

Historia hariri

Tangu karne ya 9 kuna taarifa kuhusu milki kubwa iliyokuwa na mji mkuu katika Gao. Milki ya Gao ilikuwa na utajiri kutokana na udhibiti wake juu ya uchimbaji wa chumi na biashara yake. Ilifuatwa na Milki ya Songhai iliyotumia pia Gao kama mji mkuu. Uvamizi wa Moroko katika karne ya 16 ulimaliza milki hiyo.

Mkoa wa Gao ndani ya Mali hapo awali ulijumuisha sehemu nzima ya nchi iliyopo upande wa mashariki mwa Mkoa wa Timbuktu. Mnamo 1991 nusu ya kaskazini ya Mkoa wa Gao ikatengwa na kuwa Mkoa wa Kidal .

Wakati wa uasi wa Watuareg wa 2012, Mkoa wa Gao ulikuwa sehemu ya maeneo ya Mali ya kaskazini ambayo yalitangazwa kuwa nchi mpya ya Azawad na Harakati kwa Ukombozi wa Azawad (MNLA). Katika mapigano ya Gao kwenye Juni 2012 wanamgambo Waislamu walishinda MNLA wakatawala mkoa hadi kufukuzwa na jeshi la Kifaransa.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. Communes de la Région de Gao, Ministère de l'administration territoriale et des collectivités locales, République du Mali, ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-16 .