Mkombozi mshiriki (kwa Kilatini: Co-Redemptrix au Coredemptrix; kwa Kiingereza: Co-Redemptress) ni sifa ya Bikira Maria kadiri ya teolojia ya Wakatoliki kadhaa, si wote[1][2][3] katika kuchunguza nafasi yake katika historia ya Wokovu.[4]

Stabat Mater kadiri ya Gabriel Wuger, 1868.

Wanaotumia neno hilo wanamaanisha kuwa Maria alishiriki kwa namna ya pekee[5] [6] kazi ya ukombozi iliyofanywa na Mwanae, Yesu Kristo, Mwokozi pekee[7], kwa kuwa Maria pia alikombolewa naye, isipokuwa alikombolewa vizuri kuliko wengine wote.

Ni kwamba Maria alitupatia kielelezo cha kuungana na mateso ya Mwana na kutoa fidia kwa ajili yetu. Alikubali kifodini cha Mwanae mpenzi ambaye alimuabudu kwa haki na kumpenda kwa hisani isiyosemeka. Shujaa kuliko Abrahamu aliyekuwa tayari kumchinja Isaka, Maria alipomtoa Mwanae kwa wokovu wetu alimuona akifa kwa mateso ya kutisha ya mwili na roho. Hakuna malaika aliyeingia kati kuisimamisha sadaka ya Maria na kumuambia, “Sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee” (Mwa 22:12). Maria aliona ilivyotimia sadaka ya Yesu, ambayo sadaka ya Isaka ilikuwa kidokezo chake tu, akateseka kwa ajili ya dhambi kadiri ya upendo wake kwa Mungu anayechukizwa nazo, kwa Mwanae aliyesulubiwa nazo, na kwa roho zetu zinazoangamizwa nazo. Kwa kuwa upendo wa Bikira ulizidi ule wa Abrahamu, maneno aliyoambiwa babu huyo yanamfaa zaidi Mama wa Kanisa: “Kwa kuwa umetenda neno hili… katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni” (Mwa 22:16-17).

Tanbihi hariri

  1. Smith, Harrison, "René Laurentin, Catholic scholar who studied visions of Mary, dies at 99", The Washington Post, September 18, 2017
  2. Joseph Cardinal Ratzinger, God and the World: A Conversation with Peter Seewald. Ignatius Press, San Francisco, 2002, p. 306
  3. San Martín, Inés. "Once again, Pope Francis says Mary is not the 'co-redemptrix'". Crux Now. Iliwekwa mnamo 25 March 2021.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. Most, Fr. William. Church Teaching on Mary's Co-Operation in the Redemption of Mankind Retrieved March 26th, 2020.
  5. "ZENIT - Why It's Not the Right Time for a Dogma on Mary as Co-redemptrix". 2008-09-28. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-09-28. Iliwekwa mnamo 2017-07-08.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
  6. “Therefore, one can say, she [that is, the Blessed Virgin] redeemed with Christ the human race.” Pope Benedict XV, Apostolic Letter Inter soldalica, AAS 1918, 181.
  7. St. Ambrose, De inst. virg. 7, cited from Ott, Dogmatics.

Marejeo hariri

  • Ludwig Ott, Fundamentals of Catholic Dogma, Mercier Press Ltd., Cork, Ireland, 1955.
  • Acta Apostolicae Sedis, referenced as AAS by year.

Viungo vya nje hariri