Mkubayoka

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Colubridae (Nyoka walio na mnasaba na kipiri)
Oppel, 1811
Nusufamilia: Natricinae
Bonaparte, 1838
Jenasi: Natriciteres
Loveridge, 1953
Ngazi za chini

Spishi 6:

Wakubayoka ni spishi za nyoka wasio na sumu za jenasi Natriciteres katika familia Colubridae. Wamepewa jina hili kwa sababu hufikiriwa kuwa feli mbaya (ukuba).

Nyoka hawa ni wafupi. Majike ya spishi kadhaa yanaweza kufika sm 54 lakini madume ni wafupi zaidi na urefu wa wastani ni kati ya sm 20 na 35. Kichwa chao ni kidogo. Rangi yao kijani, kijani-zeituni, kahawia-zeituni, kijivu au takriban nyeusi. Mara nyingi kuna mlia mpana mgongoni wenye rangi kali au angalau rangi isiyoiva.

Wakubayoka huishi karibu na maji na hula vyura na [[samaki] wadogo.

Nyoka hawa hawana sumu na kwa hivyo wanaweza kukamatwa bila hatari.

Spishi

hariri

Marejeo

hariri
  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkubayoka kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.