Mlangobahari wa Florida
Mlangobahari wa Florida (kwa Kiingereza: Straits of Florida) ni sehemu ya bahari inayotenganisha jimbo la Florida (Marekani) upande wa kaskazini na Kuba upande wa kusini.
Upana wake ni kilomita 150 baina ya visiwa vya Florida Keys na Kuba yenyewe. [1]
Maji yake huunganisha Ghuba ya Meksiko na Atlantiki.
Kati mlangobahari huo unapita mkondo wa Florida unapeleka maji ya vuguvugu kutoka Ghuba ya Meksiko kuelekea kaskazini-mashariki. Maji hayo ni chanzo kikuu cha Mkondo wa Ghuba unaotawala tabianchi za sehemu kubwa za Ulaya.[2]