Mlangobahari wa Yucatan
Mlangobahari wa Yucatan (kwa Kihispania: Canal de Yucatán, kwa Kiingereza: Yucatan Channel) ni sehemu nyembamba ya bahari iliyopo kati ya Rasi ya Yucatan ya Mexiko upande wa magharibi na Kisiwa cha Kuba upande wa mashariki.
Unaunganisha Bahari ya Karibi na Ghuba ya Mexico. Upana wake ni takribani kilomita 200 na kina chake kirefu kinafikia mita 2,800.