Mnara wa taa wa Ra's Bir

Jengo nchini Djibouti

Mnara wa taa wa Ra's Bir unapatikana nchini Jibuti, ukiunganisha Bahari Nyekundu na Ghuba ya Aden. Ni mnara wa pili unaopatikana katika eneo la Ra's Bir, rasi inayopatikana kaskazini mwa ghuba ya Tadjoura.

Historia hariri

Mnara wa kwanza wa taa wa Ra's Bir ulimalizika kujengwa mnamo mwaka 1889 ila kwa sasa mnara huu unatumika kama kituo cha kuongoza Ndege. Mnamo mwaka 1952 mnara mpya ulijengwa karibu kabisa na mnara wa kwanza ukiwa na urefu wa mita 50. Mabaharia na wavuvi kutoka katika Bahari Nyekundu na Ghuba ya Uajemi walikuwa wakionekana umbali wa maili 20 kutoka katika eneo la mnara huu.[1]

Kwa sasa, mnara huu umekarabatiwa na mamlaka ya Bandari ya nchi ya Jibuti na kusajiliwa chini ya International Admiralty na kupewa namba D7272 na pia mnara huu unatambulika na shirika la National Geospatial-Intelligence Agency (NGA) na kupewa namba 113-30952.

Marejeo hariri

  1. Agency, National Geospatial-Intelligence (2007). Sailing Directions - Enroute. ProStar Publications. pp. 166–. ISBN 978-1-57785-760-0.