Mnjugu Hausa
(Macrotyloma geocarpum)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Fabales (Mimea kama mharagwe)
Familia: Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Nusufamilia: Faboideae (Mimea inayofanana na mharagwe)
Jenasi: Macrotyloma
(Wight & Arn.) Verdc.
Spishi: M. geocarpum
(Harms) Marechal & Baudet

Mnjugu Hausa (Macrotyloma geocarpum) ni mmea wa mazao wa nusufamilia Faboideae katika familia Fabaceae. Kama mnjugu wa kawaida vikonyo vya matunda machanga huingia ardhini na makaka yanakomaa chini. Mbegu zake, zinazoitwa njugu Hausa, zipo mbili mbili ndani ya makaka. Asili ya mmea huu ni Afrika ya Magharibi. Hukuwza katika nchi mbalimbali za eneo hili, kwenye Benin hasa.


Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mnjugu Hausa kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.