Marsupialia
Mtoto mchanga wa kangaruu katika mbeleko akinyonya
Mtoto mchanga wa kangaruu katika mbeleko akinyonya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Mammalia (Wanyana wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Nusungeli: Theria
Ngeli ya chini: Marsupialia
Illiger, 1811
Ngazi za chini

Oda 7:

Wanyamapochi ni wanyama wa ngeli ya chini Marsupialia ambao wanazaa wadogo wao katika hali changa sana yaani baada ya muda mfupi wa mimba. Baada ya kuzaa wanaendelea kubeba wadogo ndani ya pochi au mbeleko ya ngozi iliyopo nje ya mwili juu ya tumbo. Humo kuna maziwa ambako wadogo wanaweza kunywa ilhali wanatunzwa vizuri na kukaa joto. Kadri wadogo wanavyokua wanaanza kutazama mazingira kutoka mbeleko na pia wanaanza kutembea nje wakirudi tena mbelekoni hadi wamefika umri wa kutosha wanaondoka.

Spishi zilizo nyingi ziko Australia na visiwa vya karibu kama Nyugini. Nyingine zinatokea Amerika ya Kusini. Wanyamapochi wanaojulikana zaidi ni kangaruu.

Mwainisho

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: