Mohammed bin Rashid Al Maktoum

Kigezo:Infobox prime minister

Mohammed bin Rashid Al Maktoum

Mohammed bin Rashid Al Maktoum (kwa Kiarabu: محمد بن راشد آل مكتوم; Muḥammad bin Rāshid al Maktūm pia Sheikh Mohammed, (amezaliwa 15 Julai 1949) ni Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE), na Emir wa Dubai.

Kazi ya kibiashara na kisiasa

hariri
Familia ya Wakuu ya Dubai
 

HH The Emir Sheikh
HH Sheikha Hind

  • HH The Hereditary Prince
  • HH Sheikha Hassa
  • HH Sheikh Rashid
  • HH Sheikh Maktoum
  • HH Sheikh Ahmed
  • HH Sheikh Saeed
  • HH Sheikha Latifa
  • HH Sheikha Sheikha
  • HH Sheikha Maryam
  • HH Sheikha Fatima
  • HH Sheikha Salamah
  • HH Sheikha Shamma

HRH Princess Haya of Jordan


Watoto wa Wake wanaojulikana:

  • HH Sheikha Manal
  • HH Sheikh Marwan
  • HH Sheikha Maitha
  • HH Sheikha Shamsa
  • HH Sheikh Mansour
  • HH Sheikh Majid

Tarehe 3 Januari 1995, Sheikh Maktoum bin Rashid Al Maktoum alisaini amri mbili ambazo zilimteua Sheikh Mohammed kama Mkuu Mteule wa Dubai.

Sheikh Mohammed alisimamia maendeleo ya miradi mbalimbali Dubai ikiwemo kuumbwa kwa Visiwa vya Palm na hoteli ya anasa ya Burj Al Arab. Pia anaendeleza ujenzi wa Burj Khalifa ambayo sasa ni muundo mrefu zaidi duniani, ufunguzi rasmi ni Jumatatu, 4 Januari 2010. Katika umiliki wake kama Mkuu Mteule, alianzisha Dubai Holding, kampuni ambayo iko na uwekezaji na biahsra mbalimbali. Sasa anamiliki asilimia 99.67 ya kampuni.[1]

Baada ya muongo wa utawala usio na ubishi,[2] yeye akawa mtawala wa Dubai tarehe 4 Januari 2006 baada ya kifo cha ndugu yake [2] Sheikh Maktoum bin Rashid Al Maktoum[2]. Pia aliteuliwa na Rais wa UAE, Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan, kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wa UAE tarehe 5 Januari 2006. Wajumbe wa Baraza la Taifa la Shirikisho la UAE waliyakubali mapendekezo ya Rais muda mfupi baadaye.

Mishango ya Hisani

hariri

Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum amejulikana kwa michango yake mikubwa Tarehe 19 Mei 2007, alitangaza mipango ya kutoa $ 10bn dola na kuanzisha shirika la usaidiza la Mohammed bin Rashid Al Maktoum, shirika la usaidizi la elimu katika Mashariki ya Kati, moja ya michango ya hisani kubwa zaidi katika historia.[3] Sheikh Mohammed alisema kuwa fedha hizo ni za kuweka daraja la kuziba pengo la maarifa kati ya Uarabuni na Kanda zilizoendelea, kuboresha kiwango cha elimu na utafiti katika kanda, kuendeleza mipango ya uongozi kwa vijana, na kuchochea ajira. Tangazo hili lilifanywa mwaka 2007 katika World Economic Forum nchini Jordan. Jumla ya thamani yake halisi kwa sasa, Hata hivyo, inasemekana kuwa tu $ 16bn.

Dubai Cares

hariri

Mnamo Septemba 2007, alianzisha kampeni ya Dubai Cares ya kutafuta pesa ili kuwaelimisha watoto milioni 1 katika nchi maskini. Kampeni hii ni mchango wa Dubai katika Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Kimataifa ya kutoa Elimu ya Msingi kwa kila mtoto kwa mwaka 2015. Kiasi kilichochangiwa kampeni hii hadi sasa kimezidi bilioni AED 3.4 (Inakadiriwa US $ 910 milioni).

Noor Dubai

hariri

3 Septemba 2008, Sheikh Muhammad pia alizindua mpango mpya wa Ramadan kwa jina "Noor Dubai", kwa lengo la kusaidia Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Kimataifa la Kuzuia Upofu (IAPB) katika kufikia malengo yake yaliyoainishwa katika VISION 2020: Haki ya Kuona. Noor Dubai itatibu na kutoa huduma za afya kwa watu milioni moja wanaosumbuliwa na shida za kuona zinazoweza kurekebishwa na upofu katika nchi zinazoendelea kwenye mitaa, kikanda, na kimataifa.

Thamani ya mali yake kwa jumla

hariri

Mwezi Juni 2009, mali yake ilikadiriwa dola 12 bilioni.[4]

Sakata

hariri

Tarehe 9 Machi 2007, gazeti lililo na makao yake mjini London la Metro ilichapisha picha ya Sheikh Mohammed kimakosa, ikirejerea mtuhumiwa wa ugaidi Khalid Sheikh Mohammed. The Metro iliomba msamaha kwa makosa.[5]

Sheikh Mohammed ametuhumiwa kwa kuhimiza utekaji nyara na utumwa wa maelfu ya wavulana kwa ajili ya matumizi kama walezi wa ngamia katika mashindano ya ngamia. Kesi ya watu wengi imepelekwa kortini Marekani kuhusu jambo hili.[6][7][8] Hata hivyo, mwaka 2006, UAE ilipeleka kesi ya kuondolewa kwa mashtaka haya kwa sababu si tu hakuna vyama-husika vilivyo na makazi nchini Marekani, lakini pia kuwa na uwezekano wa kumwagia maji juhudi za UAE za kushirikiana na UNICEF ili kukabiliana na tatizo hili. Tangu mwaka 2005, jitihada hizi za pamoja zimehakikisha mamia ya watoto kulipwa fidia, kupewa elimu na kadhalika baada ya kurudi makwao. Serikali ya UAE ilitumia $ 2.7 milioni mwaka 2005 na ufadhili wa nyongeza ya dola milioni 9 katika awamu ya pili ambayo inatoa fidia na vifaa nchini Pakistan, Sudan, Mauritania, na Bangladesh. Kulazimisha ufuataji wa sheria hii, sheria ya kupiga marufuku na adhabu ya muda kwa jela na faini $ 27.200.[9] UNICEF walisifu juhudi za UAE na kueleza hadharani matumaini yao kuwa "Programu ya UAE itatumika kama mfano wa kuigwa kwa nchi nyingine katika kanda, kama njia ya kukomesha aina zote za unyonyaji wa watoto".[10]

Mnamo Julai 2007, kesi iliondolewa na jaji Cecilia Altonaga aliyesema kuwa kesi haikuwa inahusika katika mahakama ya Marekani.

Marejeo

hariri
  1. [3] ^ "Maelezeo mafupi ya Dubai Holding", Zawya.
  2. 2.0 2.1 2.2 [4] ^ Ripoti ya BBC, 2006/01/05
  3. "Dubai ruler in vast charity gift", BBC News, 2007-05-19. Retrieved on 2007-05-19. 
  4. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-29. Iliwekwa mnamo 2012-05-29.
  5. Sheikh Mohammed kuomba msamaha, Metro News, Ijumaa 9 Machi 2007
  6. [9] ^ Wakuu wa dubaiwatuhumiwa kwa kuwa viongozi wa uuzaji wa watumwa wa kutunza farasi - Americas, World - The Independent
  7. [10] ^ BBC NEWS | Mashariki ya Kati | Mtawala wa Dubai atuhumiwa kwa utumwa
  8. [11] ^ Kiongozi wa Dubai aangalia kesi ya utumwa - 14 Septemba, 2007 - The New York Sun Ilihifadhiwa 13 Oktoba 2012 kwenye Wayback Machine.
  9. [13] ^ Uhusiano wa UAE-US; http://www.uae-us.org/page.cfm?id=63 Ilihifadhiwa 29 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.
  10. [14] ^ Tovuti ya UNICEF http://www.unicef.org/media/media_26692.html Ilihifadhiwa 10 Mei 2012 kwenye Wayback Machine.

Marejeo zaidi

hariri
  • My Vision - Challenges in the Race na Mohammed bin Rashid Al Maktoum (2006); katika Kiarabu; anaelezea maono ya Sheikh Mohammed ya Dubai
  • Dubai The Maktoum Story na John M. Smith; katika Kiingereza; kitabu kinachotuhumu utawala wa Sheikh Mohammed

Viungo vya nje

hariri
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
 
WikiMedia Commons
Mohammed bin Rashid Al Maktoum
Born: 1949
Regnal titles
Alitanguliwa na
Maktoum bin Rashid Al Maktoum
Ruler of Dubai
2006–present
Incumbent
Ofisi za Kisiasa
Alitanguliwa na
Maktoum bin Rashid Al Maktoum
Waziri Mkuu wa Falme za Kiarabu
2006–present
Incumbent