Maktoum bin Rashid Al Maktoum

Maktoum bin Rashid Al Maktoum (1943 - 4 Januari 2006) (Kiarabu: مكتوم بن راشد آل مكتوم) Maktūm bin Rāshid al-Maktūm pia anajulikana kama Sheikh Maktoum (jina la heshima) alikuwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Emir au mtawala wa Dubai.

Maktoum bin Rashid Al Maktoum
مكتوم بن راشد آل مكتوم


Muda wa Utawala
9 Desemba 1971 – 25 Aprili 1979
Rais Zayed bin Sultan Al Nahyan
aliyemfuata Rashid bin Saeed Al Maktoum
Muda wa Utawala
7 Oktoba 1990 – 4 Januari 2006
Rais Zayed bin Sultan Al Nahyan
Khalifa bin Zayed Al Nahyan
mtangulizi Rashid bin Saeed Al Maktoum
aliyemfuata Mohammed bin Rashid Al Maktoum

tarehe ya kuzaliwa 1943
Dubai, Falme za Kiarabu (then a colony of the Ufalme wa Muungano)
tarehe ya kufa 4 Januari 2006 (miaka 63)
Dubai, Falme za Kiarabu
utaifa Emirati
ndoa Sheikha Alia bint Khalifa bin Saeed al Maktoum
dini Sunni Islam

Maisha

hariri

Mzaliwa wa Al Shindagha, Dubai kwa familia ya Al Maktoum, kabila ya Al Bu Falasah, alikuwa Waziri Mkuu mara ya kwanza tarehe 9 Desemba 1971 na kutumikia hadi 25 Aprili 1979 wakati nafasi yake ilichukuliwa na baba yake, Sheikh Rashid Bin Saeed Al Maktoum. Kufuatia kifo cha babake 7 Oktoba 1990 aliichukua nafasi yake kama Waziri Mkuu na kama mtawala wa Dubai. Alitumikia katika nyadhifa zote mbili hadi kifo chake tarehe 4 Januari 2006.

Sheikh Maktoum pia aliwahi kuwa Rais wa Falme za Kiarabu tarehe 2-3 Novemba 2004 kufuatia kifo cha Sheikh Zayed bin Sultan Al Nahyan mpaka Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan alipotangazwa kama Rais wa Muungano wa Falme za Kiarabu tarehe 4 Novemba 2004.

Sheikh Maktoum aliongoza Dubai pamoja na ndugu zake wawili, Sheikh Mohammed (Mkuu mteule na Waziri wa Ulinzi) na Sheikh Hamdan (Waziri wa Fedha) wa United Arab Emirates. Kimataifa, alijulikana kama mmoja wa wenyewe (pamoja na ndugu zake) wa kampuni ya Dubai ya Godolphin Stables ambayo ilishindana katika mashindano makubwa ya farasi ulimwenguni.

Sheikh Maktoum bin Rashid Al Maktoum alifariki asubuhi ya 4 Januari 2006, baada ya 'heart attack' kama amekaa katika hoteli ya Palazzo Versace iliyo katika Gold Coast, Queensland, Australia. Nafasi yake ilichukuliwa na ndugu yake, Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum kama mtawala wa Dubai.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
Alitanguliwa na
Zayed bin Sultan Al Nahyan
President of the UAE (acting)
2004
Akafuatiwa na
Khalifa bin Zayed Al Nahyan
Alitanguliwa na
-
Prime Minister of the United Arab Emirates
1971—1979
Akafuatiwa na
Rashid bin Said al-Maktoum
Alitanguliwa na
Rashid bin Said al-Maktoum
Prime Minister of the United Arab Emirates
1990—2006
Akafuatiwa na
Mohammed bin Rashid Al Maktoum
Alitanguliwa na
Rashid bin Said al-Maktoum
Emir of Dubai
1990—2006
Akafuatiwa na
Mohammed bin Rashid Al Maktoum
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maktoum bin Rashid Al Maktoum kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.