Alfabeti ya Morse

(Elekezwa kutoka Morse code)

Alfabeti ya Morse (msimbo wa Morse) ni namna ya kuwasilisha herufi, namba au alama nyingine kwa kutumia mahadhi.

Alfabeti ya Morse na namba zake.
Alfabeti ya Morse bado inatumika kwenye meli na manowari, kwa kutumia taa.

Msimbo wa Morse inatumia nukta na mistari, au alama mbili, moja fupi na nyingine ndefu zaidi.

Alfabeti ya Morse imepata jina lake kutoka Samuel Morse, anayekumbukwa kama mbuni wake. Haitumiwi sana leo kama ilivyokuwa katika karne ya 19 na 20. Tangu karne ya 20 teknolojia tofauti zimechukua nafasi yake.

Kuna aina tofauti za msimbo wa Morse kwa nchi tofauti.

Kuna alama tatu tofauti katika msimbo wa Morse; kuna fupi, kawaida huitwa 'dit', ndefu, inayoitwa 'dah', na kituo. Dah ni ndefu mara tatu kuliko "dit", na kituo huwa na urefu sawa na "dit".

Njia tofauti za kutuma msimbo wa Morse

hariri

Msimbo wa Morse unaweza kutumwa kwa njia tofauti. Kwenye meli, taa zinazoangaza mara nyingi zilitumika badala ya mawasiliano ya redio.

Viungo vya Nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.