Mpasuambegu
Mpasuambegu michirizi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Fringillidae (Ndege walio na mnasaba na chiriku)
Jenasi: Crithagra
Swainson, 1827
Ngazi za chini

Spishi 17:

Wapasuambegu ni ndege wadogo wa jenasi Crithagra katika familia Fringillidae. Spishi nyingine za Crithagra ambazo zina rangi njano na/au nyekundu huitwa chiriku. Wapasuambegu wana rangi ya kahawa, kijivu na nyeupe na pengine njano kidogo na wana michirizi myeusi. Hawa ni ndege wa maeneo yenye miti. Hula mbegu lakini hulisha makinda yao wadudu. Hujenga tago lao kwa manyasi, nyuzinyuzi na pengine vigoga na kuvumwani katika panda ya mti. Jike huyataga mayai 2-5.

Spishi za Afrika hariri

Spishi za Asia hariri

Picha hariri